• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUUSHEREHEKEE UHURU WA TANZANIA BARA KWA KILIMO CHENYE TIJA _ DAS MOMBA

Imewekwa : December 9th, 2022

Katibu tawala Wilaya ya Momba Bi. Mary Marco ameyasema hayo katika Sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara zilizo fanyika kiwilaya katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tunduma TC iliyopo kata ya Maporomoko ndani ya Halmashamauri ya Mji Tunduma

Katika Maelezo yake Katibu tawala amewaeleza wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo kuwa

“Kipindi cha miaka 61 (1961 – 2022) katika Sekta ya kilimo Wilaya ya Momba imepata mafanikio mengi ikiwemo uzalishaji wa mazao ya chakula ya kujitosheleza, na ongezeko la mazao ya biashara kama Alizeti, Ufuta, Uwele, Mtama Na Mpunga. Mabadiliko makubwa katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika kilimo (zana za           Kilimo, Pembejeo, Mbolea, Mbegu bora na   hifadhi bora ya mazao kupitia maghala yaliyojengwa). Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kufikia tani 187,808.05 mwaka 2021/2022 ambayo ni mazao Ya Mahindi, Mpunga, Mtama, Uwele, Muhogo, Viazi Vitamu, na Maharage” alisema Katibu Tawala

Uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo ni Alizeti, Ufuta, Ulezi na Uwele umeongezeka na kufikia tani 29,307 mwaka 2021/2022. 

  

Pia Katibu tawala aliendela kueleza kuwa kwa miaka 61 sasa matumizi ya zana za kilimo yameboreshwa.

“Mwaka 1961 hadi mwaka 1975 matumizi ya zana bora yalikuwa duni na hivyo kazi nyingi za kilimo zilifanyika kwa kutumia jembe la mkono na wanyamakazi kwa kiasi kidogo.  Mwaka 2012/2013 Wilaya ilikuwa na jumla ya matrekta makubwa 1, matrekta madogo 2 na majembe ya kukokotwa na wanyamakazi 414 Mwaka 2021/2022, zana hizi zimeongezeka hadi kufikia matrekta makubwa 8, matrekta madogo 24” alisisitiza Katibu Tawala

Eneo linalolimwa kwa lengo la uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka. Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa eneo linalolimwa limeongezeka kufikia hekta 129,137 Mwaka 2021/2022. Matumizi ya mbolea ya viwandani kutoka tani 293 mwaka 2013 hadi kufikia wastani wa tani 13,913.6 kwa mwaka 2021/2022.

Aidha katibu tawala alisisistiza umuhimu wa wananachi kutumia kikamilifu fursa nyingi zilizopo za uwekezaji ambazo tukizitumia vizuri tutaweza kuondoa umaskini wa kipato na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wa Wilaya ya Momba, Kiuchumi na Kijamii.  Kwa miaka sitini ijayo tuongeze nguvu katika kufanya kazi kwa bidii, kutumia kikamilifu rasilimali tulizo nazo kwa kuzalisha zaidi bidhaa zilizoongezwa thamani na kutumia fursa za masoko zilizopo ikiwa ni pamoja na matumizi mazuri ya rasilimaliwatu, ardhi na teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya Mkoa na Taifa kwa ujumla

Mwisho: Katibu tawala aliwashukuru wana umoja wa Mbeya Kwanza Project kwa kujitoa kwao katika kuadhimisha Sherehe za uhuru wa Tanzania Bara kwa kuwanunulia mahitaji mbalimbali Watoto wenye uhutaji maalumu. Katika maadhimisho hayo umoja wa Asante Mbeya Project ulitoa vitu vyenye thamani ya Tsh. 2,005,500/= ikiwemo Magodoro, Mchele, Unga Wa Semge, Madaftari, Chumvi, Sukari, Sabuni na Taulo za Kike.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa