• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

UTAMBUZI WA MIFUGO KWA HERENI ZA KIELEKTRONIKI UMESITISHWA KWA MUDA_Majaliwa

Imewekwa : November 3rd, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha kwa muda wa miezi mitatu zoezi la utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kielektroniki wakati ikiendelea na tathmini ambayo itawezesha kutoa muongozo wa namna bora zaidi ya kutekeleza zoezi hilo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema bei elekezi ya kuweka hereni za kielektroniki kwa mnyama mmoja ni shilingi 1,750 kwa ng’ombe na punda na shilingi 1,000 kwa mbuzi na kondoo. ’’Gharama hizi zimekuwa zikilalamikiwa na wafugaji kuwa ni kubwa tofauti na uhalisia.’’

’’Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imesikia hoja za wafugaji kuhusu mapungufu ya kanuni, usimamizi wake na utekelezaji wake na gharama kubwa za uwekaji hereni za kielektroniki na inaona kuna haja ya kufanya upya tathmini ya zoezi hilo.’’

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 3, 2022) Bungeni jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa zoezi la utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kielektroniki na kuzuka kwa moto katika hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.

Amesema kuwa zoezi la utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kielektroniki lilipaswa kukamilika tarehe 31 Oktoba, 2022 lakini hadi kufikia tarehe hiyo idadi ya mifugo iliyotambuliwa na kusajiliwa ni 5,068,617 sawa na asilimia 11 ya lengo la kutambua mifugo 45,920,000.’’

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali haijasitisha malipo kwa ajili ya huduma hiyo bali wamesitisha zoezi linalolalamikiwa ili kuipa nafasi Serikali kupitia Wizara ya Mifugo kufanya tathmini ya mapungufu ya kikanuni yaliyowekwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo vizuri kwa kushirikisha wadau wa mifugo.

Amesema Serikali imefanya juhudi kubwa kuibadili sekta hiyo kwa kufungua soko la nyama katika nchi mbalimbali, kuondoa tozo kero na kuweka ruzuku kwenye dawa za kuogeshea mifugo na ujenzi wa mabwawa na malambo. 

’’Natoa wito kwa wafugaji wote nchini kufuga kisasa ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa nyama na mazao mengine kwa ajili ya masoko na uchakataji wa ndani na nje ya nchi.’’


Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza Wizara za Maji, Mifugo na Uvuvi na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya mifugo kuhakikisha miradi mikubwa ya maji inayotekelezwa kwenye maeneo yenye shughuli za wafugaji inafanyiwa tathimini na kupewa kipaumbele cha kutengeneza miundombinu kwa ajili ya mifugo ikiwemo maeneo ya kunyweshea badala ya kuiacha mifugo kwenda kwenye mabonde yaliyohifadhiwa.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa maagizo matatu kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na TANAPA katika kukabiliana na changamoto ya moto kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo mlima Kilimanjaro wakati inapojitokeza.

’’Hakikisheni mnaunda kitengo ndani ya TANAPA cha kukabiliana na majanga au maafa yanayotokea ndani ya hifadhi. Pia wekezeni kwenye matumizi ya teknolojia ya kisasa hususan katika tahadhari, utambuzi na uzimaji moto pamoja na kuimarisha shughuli za doria na uokoaji kwa kushirikisha jamii na wadau.’’

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuboresha uwezo wa kupambana na majanga kwa kuimarisha sheria za mifumo ya kitaasisi na kutoa mafunzo ya pamoja miongozi mwa vyombo ndani na nje ya nchi. Pia wakati wote itahakikisha upatikanaji wa vifaa vya tahadhari, uokozi na kutoa huduma mapema kwa waathirika.

 Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkoa wa Kilimanjaro, Majeshi, TANAPA, taasisi nyingine za Serikali pamoja na zisizo za Serikali, wananchi wa vijiji vya jirani na hifadhi pamoja na wadau wote walioshiri katika kikamilifu katika uzimaji wa moto


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa