• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Uyui DC Watembelea Tunduma Kujifunza

Imewekwa : October 30th, 2023

Na Benton Nollo, Tunduma.

Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora tarehe 30 Oktoba 2023 wametembelea Mji wa Tunduma kwa ziara ya siku moja kwa lengo la kujifunza mikakati inayotumiwa na Halmashauri ya Mji Tunduma katika ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kupitia mapato ya ndani.

Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Mhe. Shaban Katalambula amesema pamoja na mambo mengine, ziara hiyo lengo kubwa ni kujifunza kuhusu maegesho ya magari hasa malori na namna chanzo hicho kinavyochangia mapato ya Halmashauri.

“Sisi kule Tabora Manispaa sasa imejaa, popote inapotaka kupumua, inapumulia Uyui kwa hiyo ndiyo maana tumechagua kuja hapa kujifunza wenzetu mnafanyaje…Mkoa wa Tabora sasa unafunguka kwa Reli ya Standard Gauge na barabara za lami zote.” Amesema Mhe. Katalambula na kuongeza;

“Kwa hiyo kwa fursa hiyo ya maegesho, tunaona kitakuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwani wanaotoka Kigoma wakitaka kuegesha, wataegesha Uyui, wanaotoka Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya wataegesha Uyui kwa sababu Manispaa imejaa...kwa hiyo sisi kwa Jiografia hiyo ndiyo sababu iliyotufanya tuje Tunduma kujifunza wenzetu mnafanya nini kwenye maegesho ili nasi tuige."

Aidha, Mhe. Katalambula amesema wamejifunza jambo kubwa kutokana na salamu na kaulimbiu inayotumiwa na Wanatunduma ambayo ni 'Tunduma, Lango Kuu la SADC'.

"Ndugu zangu kwa kweli tulipofika hapa moja ya jambo ambalo tumejifunza ni salamu yenu ya 'Tunduma, Lango Kuu la SADC', kwa kweli mnastahili salamu hiyo kwa kuwa mpo mpakani, na unapokuwa hapa...ninyi ndiyo mnatuwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mahusiano na SADC, yaani Tunduma mtu akija mkampokea vizuri sifa ni za Watanzania wote.. na sisi Uyui sasa ni Lango Kuu la Tabora kwa sababu ili uingie Manispaa ya Tabora kwa njia yoyote ile lazima upite Uyui." Amesema Mhe. Katalambula.

Akizungumza kwa wageni hao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayubu Mlimba amesema Mkoa wa Tabora una historia kubwa sana nchini ya kuzalisha viongozi wazuri na wachapakazi kutokana na malezi na ushirikiano wanaoupata wawapo mkoani humo.

"Nataka nisema Tabora mnajua kulea viongozi na mnapenda kujifunza, ninaye Mkurugenzi wangu Magesa hapa alitoka Tabora na alifanya kazi katika Halmashauri mbili pale na sasa ninaye Mkuu wa Wilaya naye hivi karibuni katoka Tabora. Amesema Mhe. Mlimba na kuongeza;

“Magesa katika miaka miwili aliyokaa hapa amefikisha mapato bilioni 12.7 kutoka bilioni 5.3 sasa mtu huyu mlikuwa naye ninyi huko, tafsiri yake mlimlea vizuri na ndiyo maana sisi kwa kweli tunajivunia uwepo wake...kwa sababu fedha zinazokusanya zinakwenda kutekeleza miradi na kutatua changamoto mbalimbali katika Mji wa Tunduma."

 Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa amesema ushirikishwaji wa Wakuu wa Divisheni na Vitengo wote katika zoezi zima la usimamizi na ukusanyaji wa mapato, kutumia kanzi data katika kukusanya mapato kwa vyanzo vinavyokusanywa kwa takwimu, matumizi ya Mashine za PoS na ufuatiliaji wa mara kwa mara kwenye Mfumo wa Mapato kuhakikisha fedha zilizokusanywa zinapelekwa benki ni moja ya mikakati madhubuti inayotumika katika kufanikisha zoezi la ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo.


Matukio Katika Picha

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Mhe. Shaban Katalambula akizungumza kueleza malengo ya ziara ya mafunzo iliyofanywa na Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashaurfi hiyo tarehe 30 Oktoba 2023.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayubu Mlimba akizungumza kueleza  na Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ya mkoani Tabora waliofanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 30 Oktoba 2023.

Afisa Mapato wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Dora Mbembela akiwasilisha wasilisho la taarifa ya shughuli za ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo wa Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ya mkoani Tabora waliofanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 30 Oktoba 2023.

Mkuu wa Divisheni ya Usimamizi wa Rasirimali Watu na Utawala Halmashauri ya Mji Tunduma, Selemani Kateti akiwasilisha wasilisho la Utawala Bora kwa Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ya mkoani Tabora waliofanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 30 Oktoba 2023.

 Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ya mkoani Tabora wakifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 30 Oktoba 2023.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ya mkoani Tabora waliofanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 30 Oktoba 2023.

 Picha za juu ni Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Viongozi na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ya mkoani Tabora walipotembelea maegesho ya malori inayomilikiwa na Halmashauri ya Mji Tunduma wakati ziara ya mafunzo katika Halmashauri hiyo tarehe 30 Oktoba 2023.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa