• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Uzinduzi Basi la Mnufaika Mikopo ya Asilimia 10 Wafanyika; Kuanza Safari Zake Tunduma - Mbeya

Imewekwa : May 17th, 2025

Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Momba, Silvester Lwila na Viongozi mbalimbali kwa pamoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanza safari zake, Basi Dogo la Abiria aina ya Toyota Coaster lenye Namba za Isajili T 267 ELS ambalo limenunuliwa na Mnufaika wa Mikopo ya Asilimia Kumi (10%) inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Tunduma, Brown Andengele wakati wa ziara ya kawaida ya Kamati ya Siasa ya Chama hicho Wilaya ya Momba kwa Halmashauri hiyo tarehe 17 Mei 2025.

Brown ambaye ni mlemavu, mwezi Novemba 2024 amekopeshwa na Halmashauri hiyo shilingi milioni 121.3 kwa ajili ya mradi huo ambapo katika kipindi hicho Halmashauri hiyo ilitoa mikopo ya shilingi bilioni 4.6 zinazotokana na Asilimia Kumi (10%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Wa kwanza aliyevaa miwani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo ambaye Kamati hiyo imempongeza kwa kusimamia female ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri pamoja na usimamizi mzuri wa utoaji wa mikopo hiyo kwa wahusika.

Matukio katika Picha:


Matukio Mengine katika Picha wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Momba kwa Halmashauri ya Mji Tunduma tarehe 17 Mei 2025:

Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Momba wakikagua maendeleo ya ujenzi wa moja ya madaraja sita yanayojengwa kupitia Mradi wa Kufungua Barabara ya Mpande - Machinjioni yenye urefu wa kilomita 8. Mradi huo ambao kwa mujibu wa mkataba unatekelezwa kwa muda miezi sita (kuanzia tarehe 25 Desemba 2024 hadi tarehe 25 Juni 2025) na Mkandarasi Mante Construction Company Limited kwa gharama ya shilingi milioni 425.6 za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Aidha, ufunguzi wa Barabara hiyo na ujenzi wa madaraja hayo sita unasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini - TARURA Wilaya ya Momba.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Kufungua Barabara ya Mpande - Machinjioni yenye urefu wa kilomita 8, kwa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Momba ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Silvester Lwila tarehe 17 Mei 2025.

Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Momba wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni mawlili (Wavulana bweni moja na Wasichana bweni moja) katika Shule ya Sekondari Mpande ambapo bweni moja lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 hivyo, yatawanufaisha Wanafunzi 160. Mradi huo kwa mujibu wa mkataba unatekelezwa kwa muda wa miezi mitatu na Mkandarasi Ubengwa Bulders ya jijini Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi milioni 258.7 za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Momba wakikagua ujenzi wa Zahanati mpya ya Nyerere tarehe 17 Mei 2025, ambayo tayari ujenzi wake umeshakamilika na imeanza kutoa huduma kwa Wananchi. Mradi huo mpaka kukamilika wake umegharimu shilingi milioni 64.5 ambapo Serikali ilileta shilingi milioni 50, Nguvu za Wananchi shilingi milioni 8.5, Mfuko wa Jimbo shilingi milioni 3 na Halmashauri ya Mji Tunduma kupitia mapato yake ya ndani shilingi milioni 3.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Momba ikikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Sogea - Transfoma yenye urefu wa kilometa 2 kwa kiwango cha lami, wakati wa ziara ya kawaida ya Kamati hiyo tarehe 17 Mei 2025. Baraba hiyo ambayo ujenzi wake unasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini - TARURA Wilaya ya Momba unagharimu shilingi bilioni 1.8 mpaka kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Momba ikikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 11 katika Shule ya Msingi Makambini iliyopo Kata ya Makambini. Ujenzi wa madarasa hayo unagharamu shilingi milioni 275 ambapo shilingi milioni 75 (za ujenzi wa madarasa matatu) zimetolewa na Serikali Kuu kupitia mradi wa BOOST, milioni 150 (za ujenzi wa madarasa sita) zinazotokana na Mapato ya Ndani ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na shilingi milioni 50 za kujenga madarasa mawili zimeletwa na Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu - Lanes Awamu ya Pili, ambapo ujenzi huo unafanyika kupitia njia ya "Force Account".

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa