• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Wafanyabiashara Ndogondogo Kunufaika, Vitambulisho Vilivyoboreshwa

Imewekwa : February 20th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Watendaji wa Kata 15 na Mitaa 71 ya Halmashauri ya Mji Tunduma wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Utambuzi, Usajili na Utoaji wa Vitambulisho kwa Wafanyabiashara Ndogondogo (WBN-MIS).

Mafunzo hayo yametolewa na timu ya Wataalamu kutoka Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji pamoja na Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 20 Februari 2024.

Afisa Biashara Halmashauri ya Mji Tunduma, Abutwalibu Vunja amesema kuwa vitambulisho hivyo vitatolewa kwa Wafanyabiashara Wadogodogo watakaotimiza taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kuhakikiwa, kuthibitishwa na kuruhusiwa na Afisa wa Serikali aliyeidhinishwa kwenye Mfumo.

“Mfanyabiashara atakayetimiza taratibu zote atalipia shilingi elfu ishirini tu (Tshs. 20,000/=), kisha atapatiwa Kitambulisho ambacho kitadumu kwa miaka mitatu na baada ya muda huo atapaswa kulipa shilingi elfu tano (Tshs. 5,000/=) kwa ajili ya kuhuisha kitambulisho chake” Alisema Vunja.

Naye Afisa TEHAMA, Daudi Siame amebainisha sifa ambazo Mfanyabiashara anatakiwa kuwa nazo ili kuweza kupata kitambulisho hicho kuwa ni lazima awe mkazi anayetambulika na uongozi wa mtaa/kijiji, awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA, aweze kulipia gharama ya ada ya usajili na awe na barua ya utambulisho kutoka katika Serikali ya Mtaa/Kijiji.

Siame aliongeza kuwa pamoja na vigezo hivyo pia, Mfanyabiashara huyo anapaswa kuwa anatambulika na uongozi wa wafanyabiashara katika eneo husika.

Aidha,  Afisa Maendeleo ya Jamii, Husna Mpota ameleza faida ambazo Mfanyabiashara atanufaika nazo akiwa na kitambulisho hicho kuwa ni pamoja na kutambulika na Mamlaka mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA, Jeshi la Polisi na Taasisi za Kifedha, kuweza kupata mikopo, kuhifadhi fedha na kukamilisha miamala mbalimbali ya malipo kwa njia ya kidigitali.

“Kitambulisho hiki pia kitampa Mfanyabiashara Ndogondogo kipaumbele cha kupata maeneo bora ya kufanyia biashara katika miundombinu ya masoko itakayokuwa inajengwa katika maeneo yao na kuweza kuunganishwa na mifuko ya hifadhi ya jamii” Amesema Mpota.

 Zoezi la uzinduzi wa Mfumo huo lilifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo tarehe 16 Februari 2024.

Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa