• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Wananchi Tunduma Wahimizwa Kupanda, Kutunza Miti

Imewekwa : January 11th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Wananchi katika Halmashauri ya Mji Tunduma wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupanda na kutunza miti iliyopandwa kwa ajili ya kuhifadhi mazingira ya kizazi cha sasa na cha baadaye.

Rai hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Momba ambaye ni Afisa Tarafa wa Tarafa ya Tunduma, Damson Mwamahonje baada ya zoezi la upandaji miti wakati wa ufunguzi wa Siku ya Upandaji Miti mwaka 2024 Halmashauri ya Mji Tunduma lililofanyika kwenye Msitu wa DANIDA uliopo Mtaa wa Kaloleni Kata ya Kaloleni tarehe 11 Januari 2024.

Mwamahonje amesema miti inakufa kwa sababu baada ya kupandwa jamii haikumbuki kuwa ina wajibu wa kuendelea kutunza miti hiyo isife na badala yake ikue ambapo kwa kufanya hivyo lengo mahsusi la utunzaji wa mazingira linakuwa limefikiwa kikamilifu.

“Viongozi na Wananchi wenzangu ambao leo tumeshiriki zoezi hili tutambue kuwa kupanda miti ni hatua moja lakini kuitunza miti hiyo ni hatua nyingine…tukumbuke kuwa tunapopanda miti na kuitunza ikakua, kwa pamoja tunakuwa tumefikia malengo halisi yaliyokusudiwa.” Amesema Mwamahonje na kuongeza;

“Sisi kama Serikali tutatenga siku maalum ya kukagua miti iliyopandwa mwaka jana ili tufanye tathmini na kuona kama miti hiyo ilipata matunzo yanayostahili pamoja na kuweka mifumo ya kutunza miti itakayopandwa mwaka huu na miaka ijayo ili miti hiyo isipotee bure na kufifisha juhudi tulizozitoa.”

Pia, Mwamahonje ameikumbusha na kuihimiza jamii kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji ambapo amewataka Wataalam wa Halmashauri kuzalisha miti ya kutosha na ambayo ni rafiki kwa vyanzo vya maji.

Aidha, Mwamahonje ametumia nafasi hiyo kuwaasa Wananchi kuchukua tahadhari kwa kujikinga na Ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuzingatia usafi wa mazingira. Amewaagiza Watendaji wa Mitaa na Kata kuhakikisha kuwa kila kaya ina choo na kitumike ipasavyo na amewahimiza Wananchi wasio na vyoo, kuhakikisha kuwa wanajenga mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayub Mlimba ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Momba pamoja na Wataalam wa Halmashauri kwa kusimamia vema suala la utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya kutosha.

“Mheshimiwa Mgeni Rasmi mimi pamoja na Waheshimiwa Madiwani wenzangu tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira na ninaahidi tutasimamia zoezi hili kuanzia sasa hatua kwa hatua kwenye kata, mtaa mpaka nyumba ili kuona miti hii inapandwa na kutunzwa.” Amesema Mhe. Mlimba.

Awali akisoma taarifa ya ufunguzi wa Msimu wa Upandaji Miti mwaka 2024 kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Afisa Misitu wa Halmashauri hiyo Zawadi Mwampashe amesema mpaka sasa miti 502,000 imezalishwa katika vitalu 6 huku miti 725 ikipandwa siku hiyo.

Mwampashe amesisitiza kuwa jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa kila kaya inapanda miti isiyopungua 5 ambapo ameahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa upandaji na utunzaji wa miti.


Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa