• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Wapelekeni Watoto Kuchanjwa: DC Kihongosi

Imewekwa : February 9th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi amewataka Wazazi na Walezi kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wakapatiwe chanjo kuwakinga na Ugonjwa wa Surua Rubella.

Kihongosi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Mji Tunduma kilichoketi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa Kampeni ya Taifa ya Chanjo ya Surua Rubella inayotarajiwa kuanza nchi nzima tarehe 15 hadi 18 Februari 2024.

“Kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wazazi au Walezi kupuuza jitihada za Serikali katika kuhakikisha wananchi wake wananjikinga dhidi ya magonjwa yanayoleta madhara kwa jamii ikiwemo ugonjwa huu wa Surua Rubella…magonjwa ambayo watoto wetu wasipochanjwa huenda wakapata madhara makubwa na wakati mwingine wakapoteza maisha jambo ambalo ni hasara kwa familia na taifa kwa ujumla.” Amesema Kihongosi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Mji Tunduma, Nasri Mohamed alisema lengo kuu la kampeni hiyo ni kuzuia, kuenea kwa ugonjwa wa Surua na Rubella.

“Wajumbe Kampeni hii imedhamiria kuongeza kinga kwa walengwa, hata kama wameshapata chanjo katika utaratibu wa kawaida wa kutoa huduma za chanjo.” Amesema Mohamed.

Mohamed alisema chanjo hiyo itahusisha Watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi chini ya miaka mitano (miezi 9 hadi miezi 59) na itatolewa bure kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya na maeneo maalum yaliyoandaliwa katika Halmashauri ya Mji Tunduma.

Mratibu huyo alisema Surua ni ugonjwa unaosababishwa na  virusi  vinavyoenezwa kwa njia ya hewa, ambapo dalili za ugonjwa huo ni homa, mafua, kikohozi, macho kuwa mekundu na kutoa majimaji na vipele vidogo vidogo ambavyo huanza kwenye paji la uso, nyuma ya masikio na kusambaa usoni na mwili mzima.

Pia, Mohamed alisema Ugonjwa wa Surua hukingwa kwa chanjo ya Surua ambayo hutolewa dozi mbili, mtoto anapofikisha umri wa miezi 9 na miezi 18.

Kwa upande wa Ugonjwa wa Rubella, Mohamed alisema unaosababishwa na virusi vya Rubella na kuenezwa kwa njia ya hewa na mara nyingi huwapata watoto wadogo ingawa unaweza kumpata mtu wa umri wowote na dalili zake hufanana na dalili za Ugonjwa wa Surua.

Surua na Rubella ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa chanjo kwani yasipodhibitiwa husababisha madhara makubwa kwa afya za watoto walio na umri chini ya miaka mitano na hata husababisha vifo.

Matukio katika Picha:

Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Mji Tunduma, Nasri Mohamed akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Mji Tunduma kilichoketi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa Kampeni ya Taifa ya Chanjo ya Surua Rubella inayotarajiwa kuanza nchi nzima tarehe 15 hadi 18 Februari 2024. Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi. 

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba wakiwa katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Mji Tunduma kilichoketi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa Kampeni ya Taifa ya Chanjo ya Surua Rubella inayotarajiwa kuanza nchi nzima tarehe 15 hadi 18 Februari 2024. Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi. 

Baadhi ya Viongozi wa Dini na Kimila wakizungumza wakati kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Mji Tunduma kilichoketi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa Kampeni ya Taifa ya Chanjo ya Surua Rubella inayotarajiwa kuanza nchi nzima tarehe 15 hadi 18 Februari 2024. Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi. 

Baadhi ya Wajumbe ya Wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Mji Tunduma wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichoketi kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa Kampeni ya Taifa ya Chanjo ya Surua Rubella inayotarajiwa kuanza nchi nzima tarehe 15 hadi 18 Februari 2024. Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi. 


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa