Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ndugu Tikson Nzunda leo tarehe 01/06/2022 amefanya ziara ya siku Moja ndani ya Halmashauri ya MjiTunduma.
Akiongea na wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Amesema kuwa Tanzania kwa sasa inatakiwa kufuga kisasa ili matokeo yaonekane na sio kufuga kienyeji kama zamani
Katibu Mkuu Nzunda pia amesema Wizara imeamua kufufua vyuo vyote vilivyokuwa havifanyi kazi kwa weledi na kuamua kupeleka vijana ili wakajifunze stadi mbalimbali uzalishaji wa mifugo wenye tija.
Katika maelezo yake ndugu Nzunda alisema kwa sasa wafugaji wanatakiwa kutumia eneo dogo la uzalishaji (Zero Grazing) kwa kuwa na malisho bora na kuwepo kwa mashamba darasa ya mfano ya malisho kwa wafugaji walau hata kwa hekari moja kila kata za kimkakati ili waweze kujifunza mbinu za uzajilshaji wa malisho bora kwa chakula cha mifugo ili kuongeza uzalishaji wa Maziwa
Pia Katibu mkuu alisisitiza kuwepo mkakati wa kichimba visima vya maji na mabwawa kwa kata za kimkakati ili kuweza kuwasaida wafugaji katika kuhudumia mifugo kwa kunywesha maji safi na salama kwa mifugo yao
“Afya za mifugo zishughulikiwe kwa kudhibiti magonjwa ya Mlipuko na yasiyo ya mlipuko kwa kufanya chanjo ya mifugo ambayo inatakiwa itolewe kwa ratiba moja kwa pamoja ili Halmashauri nzima iweze kuchanja mifugo yote na kuondokana na baadhi ya mifugo kubaki na magonjwa ambayo yanaweza kusababisha magonjwa kwa mifugo mingine. Chango ya Mifugo ni Lazima na sio hiyari hivyo kila mfugaji analazimika mara ratiba ikitoka kupeleka mifugo yake kwenye Chanjo husika” alisema Nzunda
Pia katika kudhibili majongwa yatokanayo na vimelea vya kupe ni lazima kila Mfugajio aogeshe mifugo yake kwa kupeleka kwenye majosho na kama Josho halipo basi watumie Bomba la mkono kuogesha mifugo yao
Pia alishauri Kuanzishwa kwa mnada mkubwa wa mifugo na mazao ya mifugo ambao unaweza kutumika katika kuuza bidhaa ndani na nje ya nchi ukizingatia Tunduma ipo Mpakani mwa nchi za SADC
Pia alisisitiza kuwa Mifugo haitakiwi kuchungwa au kuswagwa katika barabara kwani sio tu inaharibu miundombinu ya barabara bali inakosa ubora wa afya zao, kwani imekuwa ikitembea umbali mrefu sana mfano kutoka mkoa mmoja hadi mwingine na kufanya kupata majonjwa au kuambukiza mifugo mingine katika eneo ambalo halikuwa na magonjwa
Katibu mkuu alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kuwawezesha vitendea kazi maafisa Ugani katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku hata hivyo jitihada za kuendelea kuwezesha Divisheni za uzalishaji ili ziendelee kuwa na ari ya kufanya kazi
Katika kuhitimisha Katibu mkuu alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kuweza kukusanya mapato ya Ndani kwa Zaidi ya asilimia miamoja. Kwani Halmashauri ya Mji Tunduma ilipanga kukusanya Tzs 7,600,000,000/= kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022. Hata hivyo Halmashauri ya Mji Tunduma mpaka Mei 31/2022 imeweza kukusanya kiasi cha Tzs 7,635,690,500/= ambayo sawa na 100.8%
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa