• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

MRADI WA UPIMAJI VIWANJA 600 MTAA WA MSINDE KWA FEDHA ZA MKOPO KUTOKA WIZARA YA ARDHI

Start Date: 2021-12-24
End Date: 2022-05-30

Halmashauri ya Mji Tunduma ni moja kati ya Halmashauri 54 nchini zilizokopeshwa fedha kiasi cha Sh.543,000,000/= kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) viwanja 600 katika Mtaa wa Msinde Kata ya Mpemba.Fedha hizo zilipokelewa mnamo tarehe 24/12/2022.

Eneo la Mradi lililotambuliwa lipo pembeni ya Shule ya awali na Msingi ya mchepuo wa kiingereza (New Hope) upande wa kushoto wa barabara Kuu ya Mpemba-Isongole mpaka kwenye kona ya njia panda ya barabara ya zamani ya kwenda Ileje. Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 24/12/2021 na kukamilika tarehe 30/05/2022.

 

GHARAMA YA MRADI

Mradi huu umetekelezwa kupitia Fedha za Mkopo usio na riba wa Sh. 543,000.000/= uliotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa katika kukamilisha mradi huu ni Sh. 535,416,591.20. Kiasi cha Sh 7,583,408.80 kilichobaki kitatumika katika kuboresha miundombinu ya eneo lote lenye jumla ya ekari 155.

 

HALI YA UTEKELEZAJI WA MRADI

Mradi huu umekamilika kwa asilimia 99.9. Mradi huu umetekelezwa katika hatua kuu 7 ambazo ni uhamasishaji, utambuzi na uthamini wa ardhi na mali, Upangaji, Upimaji Ardhi, ufunguzi wa barabara ndani ya eneo la mradi, kutangaza na kuuza viwanja na hatua ya mwisho ni umilikishaji.

Jumla ya viwanja 622 vyenye ukubwa na matumizi mbalimbali vimepimwa na kuidhinishwa katika eneo lililotwaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utwaaji wa Ardhi ya mwaka 1967 na kulipwa fidia ya kiasi cha Sh. 469,963,100/= kwa wananchi 101 wenye mashamba yenye jumla ya ukubwa wa ekari 155. Hatua iliyobaki ni ya umilikishaji wa viwanja hivi kwa wananchi waliogawiwa baada ya maombi yao kukubaliwa na mamlaka ya Upangaji ambayo ni Halmashauri ya Mji Tunduma, pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya eneo la mradi.

 

MANUFAA YA MRADI

Manufaa yanayotarajiwa kupatikana katika mradi huu ni kama ifuatavyo:-

  1. Kuwa na Ardhi iliyopangwa, kupimwa na kumilikishwa kisheria ikiwa ni sehemu ya   utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya Ardhi kitaifa pamoja na kupunguza migogoro ya Ardhi.
  2. Kukuza Uchumi wa Mji uliopangika kwa kuwa na maeneo ya huduma mbalimbali kama masoko, shule, maeneo ya wazi, burudani na huduma muhimu kwa jamii kama vile umeme na maji kufikika kirahisi kwa wakazi.
  3. Kutokana na mauzo ya viwanja hivi, Halmashauri ya Mji inatarajia kukusanya jumla ya Sh.1,066,974,242/=, ambazo kati ya hizo Sh. 543,000,000/= zitarejeshwa Serikali Kuu ili kulipa mkopo uliotolewa bila riba na kuifanya Halmashauri ya Mji kupata mapato ya kiasi cha Sh. 523,974,242/= kama faida na kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Mji wa Tunduma.


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa