Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando amesema atahakikisha elimu inaendelea kutolewa kwenye mikopo ya walemavu hili wajitokeze kukopa na kurudisha fedha hizo.
Mhe. Irando amesema hayo alipokuwa anaongea na walemavu wa Tunduma wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu anayeshughulikia masuala ya walemavu, Mhe. Stella Ikupa Alex, 9 Julai 2020.
Pia, Mhe. Irando amewataka walemavu wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani.
Mhe. Waziri ametembelea kikundi cha walemavu Tunduma ambao wanamiliki bajaji 4 na pikipiki ambazo wamezipata kutokana na mkopo wa 2% kutoka Halmashauri ya Mji Tunduma.
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957389
Simu ya Mkononi: +255 754 549 511
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa