• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Divisheni ya Elimu ya Sekondari


TAARIFA YA DIVISHENI YA ELIMU SEKONDARI 

 

UTANGULIZI

 Halmashauri ya Mji Tunduma ina shule za Sekondari 19 kati ya hizo shule za serikali ni 14 na 5 zisizo za serikali. Tunaishukuru sana Serikali na wananchi kwa ujumla kwa ujenzi wa shule katika kipindi kifupi kwani mwaka 2016 kulikuwa na shule 6 tu za Sekondari na kati ya hizo 5 zilikuwa za serikali na Moja tu ya binafsi. Idadi ya Wanafunzi  ni 10,244 wavulana 4,735 wasichana 5,509.



2.0 UANDIKISHAJI WA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2022

Wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 katika Halmashauri ya Mji Tunduma walipata nafasi kwa asilimia mia moja.  Tunakushukuru sana  Serikali ikiongozwa na Mh,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Wananchi kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani kujenga madarasa ya kutosha kwa kupitia programu ya UVIKO-19 kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi hawa. Takwimu za uandikishaji ni kama ifuatavyo:

Takwimu za Uadikishaji Kidato cha Kwanza 2022

Na
Waliopangwa
Wv
Ws
Jumla
%
1
1882
1860
3742
100
2
Walioripoti Shule za Serikali
1588
1720
3308
88.40
3
Walioripoti Shule Binafsi
  273
  126
  399
10.66
4
Wasioripoti
21
14
35
0.9

 

 

 

3. MAHITAJI YA WALIMU

Kwa ujumla mahitaji ya walimu wa Sekondari ni 355 na waliopo ni 267  na upungufu ni 88. Upungufu mkubwa ni kwa masomo ya Sayansi na Hisabati kama jedwali lifuatalo linavyoonesha.

MAHITAJI YA WALIMU KIMASOMO

 
MASOMO YA SANAA

 

MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

Mahitaji
Waliopo
Upungufu
Mahitaji
Waliopo
Upungufu
194
181
13
161
86
75


Tuna kila sababu ya kuishukuru Serikali kupitia ajira za Mwezi Julai 2022 ambapo Halmashauri ya Mji Tunduma tulipata walimu wa ajira mpya wapatao 33 na walioripoti ni 32 mwalimu mmoja hadi sasa hajaripoti ambaye ni wa masomo ya Sayansi na alipangiwa shule ya Sekondari Mpande. Ili kukabiliana na Upungufu tulionao Halmashauri imewaruhusu Wakuu wa Shule za Sekondari kuwapokea walimu wanaojitolea ili kupunguza uhaba wa walimu uliopo.


  • HALI YA MIUNDOMBINU

Halmashauri kwa sasa haina upungufu wa vyumba vya madarasa hii ni baada ya Serikali kujenga madarasa mengi kupitia Mradi Na TCRP 5441. Kwa mara ya kwanza Halmashauri ina ziada ya vyumba vya madarasa tofauti na miaka iliyopita, hapa tuna kila sababu ya kumpongeza sana Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Shule. Aidha, tunamshukuru Mh. Mbunge, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Mkurugenzi na timu ya Wataalamu kwa kushirikiana na wananchi katika kusimamia kujenga miundombinu ya kutosha kama ifuatavyo:

AINA YA MIUNDOMBINU

MAHITAJI

YALIYOPO

ZIADA/UPUNGUFU

Madarasa

237

287

       50  Ziada
Matundu ya vyoo

427

323

104 Upungufu

Nyumba za walimu

235

11

224 Upungufu

Viti na Meza za Wanafunzi

9320

8525

795

 

 

4.1 MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA FEDHA ZA COVID – 19 

Mwezi Oktoba, 2021 Halmashauri ilipokea jumla ya Shilingi 1,040,000,000 kupitia mradi wa COVID 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 52 katika shule za Sekondari. Miradi yote ilikamilika kwa wakati tayari madarasa yanatumika.

 

4.2 MRADI WA SEQUIP 

Katika utekelezaji wa Programu ya Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Halmashauri imepokea fedha za ujenzi wa shule mbili ikiwemo shule ya Wasichana ya Mkoa ya Kitaifa inayojengwa kata ya Chiwezi Mtaa wa Namole. Shule hii imetengewa Tsh. 4,000,000,000/= na zimepokelewa Tsh. 3,000,000,000/=. Tayari mradi umeanza kutekelezwa. Shule ya pili ni Uwanjani Sekondari ambayo imepokea Tsh.470,000,000/= na kazi za ujenzi zinaendelea.


4.3 MAPOKEZI YA FEDHA ZA ELIMU BULE

Katika kipindi cha miaka mitatu, Halmashauri ya Mji Tunduma imepokea kiasi cha Tsh.1,078,513,317.11 kwa ajili ya uendeshaji wa Shule zote za Sekondari kwa kipindi cha miaka mitatu kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo:

MWAKA
KIASI KILICHOPOKELEWA
 2019-20 
               330,759,819.12 
 2020-21 
               350,559,929.75 
 2021-22 
               397,193,568.24 
 JUMLA KUU 
               1,078,513,317.11 



5. HALI YA TAALUMA 

Kwa ujumla hali ya taaluma kwa Halmashauri imeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka kwa viwango tofauti tangu mkoa ulipoanzishwa mwaka 2016. Matokeo yote ya mitihani ya Kitaifa kuanzia Upimaji wa kidato cha Pili, Mitihani ya Taifa kidato cha Nne na cha Sita yote yanaimarika mwaka hadi mwaka kama ifuatavyo:

 
NA
 

Darasa

Asilima ya ufaulu

Mwaka 2019
Mwaka 2020
Mwaka 2021
Mwaka 2022
1
Kidato cha Pili

98.2%

98.7%

99.4%

-

2
Kidato cha Nne

94.8%

95.4%

99.2%

-

3
Kidato cha Sita

100%

99.3%

100%

100%

Aidha, kwa mwaka 2021 ufaulu uliimarika zaidi hasa kwa kidato cha Nne na   Halmashauri ya Mji Tunduma ilishika nafasi ya 6 Kitaifa na imepata tuzo ya kuwa miongoni mwa Halmashauri zilizoongeza ufaulu mfululizo kwa miaka 03 kuanzia mwaka 2019, 2020 na 2021.



6. MIKAKATI YA KUINUA TAALUMA

  • Halmashauri inasimamia mikakati ya Mkoa na Halmashauri ya kuinua taaluma Mkoana Songwe na Taifa kwa ujumla. Moja ya Mikakati mikubwa ni kufanya mitihani ya Pamoja kwa madarasa yote. Vidato vya mitihani vinafanya mitihani ya Utamilifu (mock) kimkoa lakini kidato cha Nne wamefanya Mtihani wa Kanda kwa Mikoa mitano ikiwemo Songwe, Njombe, Mbeya, Rukwa na Katavi. Katika matokeo ya mitihani hiyo Halmashauiya Mji Tunduma imeshika nafasi ya kwanza kwa Halmashauri zote za Mikoa hiyo mitano kwa ufaulu wa asilimia 98.3.


  • Mkakati mwingine ni kutoa tuzo kwa shule, walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa. Tunawapongeza Waheshimiwa Madiwani na Mkurugenzi pamoja na timu ya Wataalamu, kwa pamoja walitoa tuzo kwa walimu pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya Kitaifa. Pia tunaishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nayo imekua ikitoa tuzo na zawadi kwa shule zinazofanya vizuri hii inatoa hamasa kwa walimu na wanafunzi pia.

 

  • Utoaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi pia ni mkakati endelevu pamoja na kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa