• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji



Divisheni hii imeanzishwa mwaka Januari 2022 na utekelezaji wake umeanza rasmi Julai 2022, kabla ya hapo biashara ilikuwa kitengo kwenye Idara ya Fedha na Biashara. Divisheni hiikwa Halmashauri ya Mji wa Tunduma ina watumishi wawili tu wakudumu na watumishi watatu wa mkataba. Majukumu makubwa ya Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni:

  • kusimamia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
  • kuratibu na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara
  1. Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, na Kanuni na taratibu za Sekta za Viwanda, Biashara na Masoko katika Mamlaka ya serikali za Mitaa;
  2. Kutoa Elimu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo walioko katika sekta binafsi katika eneo lililo chini ya mamlaka .
  3. Kuwa kiungo na wizara kupokea taarifa za sera ,Seria na mikakati ya Wizara na kuzisambaza kwa wadau mabalimbali katika mamlaka za Serikali za Mitaa;
  4. Kupokea ,kuchambua na kuunganisha taarifa za usambazaji katika sekta ya viwanda, Biashara na Masoko na kutoa taarifa OWM - TAMISEMI,Wizara ya Viwanda na Biashara na kwenye Sekretariati za Mikoa na kushauri ipasavyo;
  5. Kushauri na kuratibu shughuli za usajili wa Shughuli za Biashara katika mamlaka za Serikali za Mitaa (Business Activities Registration) kwa mujibu wa sheria.
  6. Kupendekeza namna ya kuboresha mazingira wezeshi ya biashara kwa madhumuni ya kurahisisha taratibu za kuanzisha biashara nchini ;


1.0 SHERIA ZINAZOSIMAMIA SHUGHULI ZA BIASHARA 

Katika kuhakikisha shughuli za Biashara na Viwanda zinaendeshwa kwa kufuata taratibu na sheria, Serikali imeweka sheria mbalimbali kwa ajili ya kusimamia uendeshaji ya shughuli za biashara. Sheria hizo ni kama ifuatavyo:

1. Sheria ya Leseni za Biashara Na. 25 ya Mwaka 1972 ambayo imekuwa ikifanyiwa marekebisho ya mara kwa mara na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(marekebisho yamefanyika mwaka 1980, 2004, 2013) ili kuendana na wakati. 2. Leseni ya vileo Na. 28 ya Mwaka 1968 sheria hii inasimamia vileo vya Viwandani na vileo vya asili(Vilabu vya Pombe za Kienyeji) sheria hii ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Haijawahi kufanyiwa marekebisho toka kutungwa kwake.

3. Sheria ya Ushuru wa nyumba za kulala wageni(Guest house Levy ya Mwaka 1972) na marekebisho yake ya mwaka 2015

4. Sheria ya usafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki za magurudumu mawili na matatu zinazojulikana kama “the transport licensing (motor cycle and tricycles) regulation, 2010”. 5. Pamoja na Sheria mbalimbali za Mamlaka za Uthibiti(regulatory Authority) kama EWURA, SUMATRA, CRB, TFDA n.k


 2.0 SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA KUSIMAMIWA NA DIVISHENI YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI

Katika kila Halmashauri kuna Kitengo cha Biashara ambacho kinasimamia shughuli za biashara. Kitengo cha Biashara kinafanya shughuli zifuatazo:-

1. Kupokea na kupitisha fomu za maombi ya leseni za Biashara, Leseni za Vileo na usajili wa usafirishaji abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu.

2. Kutoa leseni za Biashara, leseni za Vileo na stika za usajili wa usafirishaji abiria kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu kwa mujibu wa sheria zake.

3. Ku – issue Leseni za biashara, kwenye Mfumo wa Kieletronik wa ukusanyaji Mapato. 4. Kukusanya na kusimamia mapato ya Ada za Leseni za Biashara, leseni za Vileo, usajili wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu na ushuru wa nyumba za kulala wageni

5. kufanya ukaguzi wa leseni za biashara na kutoa elimu ya Biashara ikiwa ni pamoja na sheria Na. 25 ya Mwaka 1972 na maelekezo mbalimbali yanayohusu shughuli za biashara

6. Kutoa ushauri wa Kitaalam na mafunzo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanaondesha shughuli mbalimbali za Viwanda na Biashara.

7. Kutafsiri na Kusambaza nyaraka, sera na sheria mbalimbali zinazuhusu shughuli za Viwanda. biashara, na uwekezaji kwa wafanyabiashara.

8. Kumshauri kitaalam Mkurugenzi Masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Biashara, Viwanda na uwekezaji katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.


3.0 VYANZO VINAVYOSIMAMIWA NA DIVISHENI YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI

Kitengo cha Biashara kinasimamia vyanzo vinne vya Mapato ya halmashauri ambavyo ni ada ya Leseni za Biashara,Leseni za Vileo, Ushuru wa Nyumba za Kulala wageni, Usajili wa taxi na Pikipiki na kodi ya pango la vibanda vilivyojengwa katika maeneo ya masoko na stendi . Pamoja na kusimamia vyanzo hivyo, Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  inasimamia shughuli zote za Biashara, Viwanda na Uwekezaji zinazoendeshwa katika Halmashauri.


4.1 LESENI ZA BIASHARA. 

Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.

 4.1.1 UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA 

Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN 211 kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:-

1. Cheti cha Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of Incorporation or Registration).

 2. Memorandum and Article of Allocation” kama ni Kampuni

3. Kitambulisho cha mpiga kura, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).

 4. Hati ya kiuwakili (prowess of a Honey) kama wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi.

 5. Ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.

 6. Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN) na Tax clearance. Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali , Kwa mfano (TFDA, EWURA, TAURA, CRB, TILLI) n.k

7. Masharti mengine ya kupata Leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha eg. Mgahawa inadidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake.

4.1.2 MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI 

1. Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi.

2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.

3. Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya Biashara No. 25 ya 1972

4. Mwenye leseni hatatoa huduma/bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na vyombo vinavyotumika kisheria.

5. Mwenye leseni anaweza kunyaganywa wakati wowote ikiwa itaonekana aliipata kwa njia ya udanganyifu au amekiuka msharti ya leseni.

4.1.3 MAKOSA 

1. Kuendesha biashara bila leseni.

2. Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye leseni.

3. Kutumia leseni moja kufanyia biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi.

 4. Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyeidhinishwa na Serikali.

5. Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi.

6. Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada/kodi inayostahili.

 7. Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.

4.1.4 ADHABU 

Mtu yeyote anayetenda majawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tshs. 50,000/= au kifungo kisichozidi miaka miwili (2) au faini na kifungo kwa pamoja.


 5.0 LESENI ZA VILEO

 Leseni za vileo hutolewa kwa mujibu wa sheria ya Leseni za vileo Na.28 ya Mwaka 1968 Leseni hizo hutolewa misimu miwili kwa mwaka yaani miezi sita sita( mfano msimu wa kwanza unaanza tarehe 1/10/2015 hadi tarehe 30/3/2016 na msimu wa pili unaanza tarehe 1/4/2016 hadi 30/9/2016. Hivyo leseni hutolewa kuanzia tarehe1-21 /4/2014 anayechelewa kukata leseni ndani ya kipindi cha siku 21 anatakiwa kutozwa adhabu ya 25% ya kiasi cha ada anacholipia Kwa mujibu wa sheria ya Leseni za Vileo Na.28 ya Mwaka 1968 halmashauri ndiyo yenye Mamlaka ya kukusanya mapato kwa kutoza ada ya leseni za Vileo kwenye Baa, grocery, store, maduka na vilabu vya Pombe za asili n.k.


6.0 USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (HOTEL LEVY) 

Kwa mujibu wa sheria, nyumba za kulaza wageni (Guest house, The Hotel levy Act 1972) kila Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kukata leseni ya biashara anatakiwa kulipia ushuru wa nyumba ya kulala wageni kila mwezi. Mmiliki anatakiwa kuwasilisha halmashauri kitabu cha wageni kwa ajili ya ukaguzi. Baada ya ukaguzi wa kitabu hicho, mmiliki hutakiwa kulipa asilimia 10% ya mapato yaliyopatikana katika mwezi huo. Kwa mujibu wa sheria ushuru huo hulipwa kuanzia tarehe 1-7 ya kila mwezi. Mmiliki anapochelewa kulipia katika tarehe hizo hutozwa adhabu ya asilimia 25% Mwaka 2015 sheria hii imefanyiwa marekebisho ambapo Mmiliki wa nyumba za kulala wageni atapaswa kulipia 10% ya mapato yake ya mwezi.

KARIBU TUNDUMA LANGO KUU LA SADC

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa