• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi


TAARIFA YA DIVISHENI YA  ELIMU YA AWALI NA ELIMU YA MSINGI 


UTANGULIZI

Halmashauri ya Mji Tunduma mpaka sasa ina jumla ya shule 64 kutoka shule 26 za mwaka 2016. Ongezeko hili kwa miaka 7 ni sawa na 242.3%, Kati ya shule hizo shule 49 ni za Serikali na 15 ni shule zisizo za kiserikali. Jumla  ya wanafunzi katika Shule za Serikali ni 46,943 ikiwemo wavulana 23,273 na wasichana  23,670. Idadi ya wanafunzi wa shule Binafsi 2728, wakiwemo wavulana1368 na wasichana 1360 hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wote kwa Shule  zisizo za Serikali kuwa 49,671. 


A: DIVISHENI YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

Kwa upande wa uandikishaji kwa wanafunzi wa darasa la kwanza mwaka huu 2022 walitarajiwa kuandikishwa wanafunzi 5,790 walioandikishwa ni wanafunzi 6,527 sawa na 113%, na awali waliotarajiwa kuandikishwa ni wanafunzi 4145 wakaandikishwa 4114 sawa na asilimia 99.2%

SHULE ZA MSINGI ELIMU MAALUM.

Halamshuri ya Mji Tunduma ina jumla ya  wanafunzi wenye mahitaji maalum 200 ikiwa wanafunzi 152 wapo katika shule zenye vitengo ambazo ni shule ya msingi Katete na Tunduma na wanafunzi 43 wapo katika shule 8 jumuishi ambazo ni Shule ya msingi Sogea,Majengo,Chiwezi,Chapwa,Uhuru,Maporomoko,Mpemba na Migombani.

 

 MIUNDOMBINU YA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

Halmashauri ya Mji Tunduma imejenga mabweni mawili (2) kupitia fedha kutoka serikali kuu na fedha za mapato ya ndani,Kwa sasa hatua iliyopo ni umaliziaji, Pindi ujenzi utakapokamilika tunatarajia wanafunzi wenye mahitaji maalum wataweza kulala katika bweni wakiendelea kupata Elimu katika mazingira rafiki na salama.

 

PROGRAMU ZA ELIMU YA WATU WAZIMA NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI

Halmashauri ya Mji Tunduma inaratibu program mbalimbali za EWW ambayo ni mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA).

Mwaka 2022 Halmashauri ya Mji Tunduma imeandikisha jumla ya wanafunzi 268, kundi rika I wakiwemo wavulana 127 na wasichana 141. Idadi ya wanafunzi wa MEMKWA imekuwa kubwa kutokana na changamoto ya wazazi na walezi kuhamia toka vijijini na watoto waliochelewa kuandikishwa shule kunakoathiri uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi katika umri unaotakiwa. Majedwali na 4 na 5 limechanganua wanafunzi wa MEMKWA kwa kundi rika la kwanza.0

JEDWALI NA. 4: TAKWIMU ZA WANAFUNZI WA MEMKWA KUNDI RIKA LA I (MIAKA 9-13)

NA

MKOA

HALM.

WALIOTARAJIWA (MAOTEO)

WALIOANDIKISHWA

IDADI YA WAWEZESHAJI

WAV

WAS

JML

WAV

WAS

JML

ME

KE

JML

1

SONGWE
TUNDUMA

205

205

410

127

141

268

3

9

12


MIUNDOMBINU

 

MAHITAJI

YALIYOPO

UPUNGUFU

Madarasa
1109
469
640
Matundu ya vyoo
12040
779
1261
Nyumba za walimu
1048
38
1010
Madawati
13,769
9007
4762

 


Pamoja na upungufu huo wa miundombinu Serikali yetu chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha mwaka hadi mwaka ili kupunguza changamoto ya miundombinu.


Mwaka huu tumetekeleza miradi mikubwa ifuatayo;

  • Ujenzi wa shule mpya 2 ambazo ni Shule ya Msingi Kokoto Tshs.400,000,000 toka serikali kuu Tshs 529,566,483.56 zinaongezwa toka mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo kunajengwa jengo la ghorofa lenye vyumba 10, chumba kimoja kimoja cha darasa pembeni, matundu 24 ya vyoo, jengo la utawala na nyumba 2 za walimu za 2 in 1.
  • Shule ya Msingi Melelani Tshs.250,000,000 za EP4R zimejenga vyumba ya madarasa 9 na matundu ya vyoo 30 na jengo  moja la utawala.
  • Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa jengo la ghorofa kwa shule ya msingi Haisoja
  • Fedha za EP4R ambazo zimejenga  Mabweni mawili ya watoto wenye mahitaji maalum, kila bweni liligharimu kiasi cha Tshs.80,000,000 hivyo kufanya jumla ya Tshs.160,000,000 na ongezeko Tshs 90,000,000 toka mapato ya ndani ya Halmashauri.
  • Fedha za EP4R Tshs. 559,200,000 ambazo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
  • Fedha za LANES Tshs. 163,395,000 ambazo zilitumika kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vya madarasa. Hata hivyo tumeendelea kutumia fedha za mapato ya ndani zaidi ya Bilioni mbili kwa mwaka 2021/2022 kujenga na kukamilisha miundombinu ya vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo. Tunawaomba wadau wa Elimu waendelee kuunga mkono jitihada za Serikali juu ya kutatua tatizo la miundombinu inayohitajika shuleni.


Kwa kifupi tumefanikwa Kwa mwaka 2021/2022 tumefanikiwa kujenga miundombinu ifuatayo

 Madarasa 56 na ofisi 11, Shule mbili za ghorofa, mabweni mawili ya Watoto wenye mahitaji maalum, nyumba za walimu 10 Matundu ya vyoo 94, madawati 400 yametengenezwa.

 Jumla ya Tshs 1,966,559,728.00 zimetumika, kati ya hizo Tshs 959,200,000.00 ni za EP4R, Tshs163,395,000.00 toka Serikali Kuu, Tshs.9,765,000.00 nguvu za wananchi na Tshs.690,454,950.00 toka mapato ya Ndani. Halmashauri ya Mji katika kuboresha miundombinu ya kutolea elimu imejenga shule mpya ya Mchepuo wa Kiingereza kwa mapato ya ndani

MAPOKEZI YA FEDHA ZA RUZUKU KWA MIAKA MITATU ILIYOPITA

MWAKA
RUZUKU YA WANAFUNZI
POSHO YA W/WAKUU
POSHO YA WARATIBU ELIMU KATA
JUMLA
2019/20

197,470,448.88

        81,600,000
           45,000,000
     324,070,448.88
2020/21

200,200,426.68

        81,600,000
           45,000,000
     326,800,426.68
2021/22

243,837,853.00

      108,000,000
           45,000,000
     396,837,853.00
JUMLA KUU

641,508,728.56

271,200,000

135,000,000

1,047,708,728.56

MAHITAJI YA WALIMU KWA UWIANO WA 1:45

 

MAHITAJI

YALIYOPO

UPUNGUFU

Walimu

1048

530

518

 

Kutokana na upungufu huo tuna walimu 60 wanaojitolea katika Shule mbalimbali za Mji wa Tunduma,



HALI YA KITAALUMA

Hali ya kitaaluma kwa Halmashauri ya Mji Tunduma imekuwa ikipanda mwaka hadi mwaka na tunawashukuru sana walimu wote na wadau mbalimbali kwa ushirikiano na juhudi zao kwani ndizo zinapelekea ufaulu huo kupanda kwa darasa la VII na la Nne kama jedwali linavyooneshwa hapo chini kwa miaka 3 mfululizo:-

DARASA LA VII

DARASA LA IV

 
Waliosajiliwa
Waliofanya
Waliofaulu
% za ufaulu
Waliosajiliwa
Waliofanya
Waliofaulu
% za ufaulu
2019
3149
3123
2554
81.8
6169
5839
5247
90
2020
3593
3485
3067
88
5549
5298
5105
96
2021
4258
4119
3743
90.9
5171
4893
4641
94.8

 

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI DIVISHENI YA ELIMU YA MSINGI NA AWALI

Kwenye mafanikio lazima changamoto ziwepo, zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazotukabili kwenye sekta ya elimu

  •  Baadhi ya shule kutotoa chakula cha mchana kwa wanafunzi
  • Baadhi ya wanafunzi kujihusisha na biashara ndogondogo , hali inayopelekea kutozingatia masomo.
  • Utoro wa rejareja wa baadhi ya wanafunzi.
  • Baadhi ya wazazi kuwakataza watoto wao kufanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa.
  • Mrundikano mkubwa wa wanafunzi madarasani kwa shule za Msingi
  • Upungufu wa walimu.


UTATUZI WA CHANGAMOTO

  •  Kupitia baraza la madiwani tumetunga Rasimu ya sheria ndogo ya utoaji wa chakula cha mchana shuleni ambapo Rasimu hiyo imeshawasilishwa OR- TAMISEMI.
  • Elimu imeendelea kutolewa kwa wazazi wanajamii ili kuweza kuacha kuwatumia wanafunzi kwenye biashara ndogondogo
  • Tumeendelea kutoa Elimu kwa wazazi na walezi ili kuweza kukomesha utoro wa rejareja
  • Aidha tumeendelea kuwahamasisha wazazi /wanajamii juu ya umuhimu wa Elimu.
  • Kutokana na uhaba wa vyumba vya Madarasa tumeendelea kuhamasisha jamii juu ya kujitolea nguvu kazi yao ili kutatua changamoto hiyo na kuvitumia vyumba vichache vilivyopo kwa kuweka wanafunzi zaidi ya 45 kwenye chumba kimoja.
  • Pia tumeendelea kuwa na walimu wa kujitolea ambapo mpaka sasa tuna jumla ya walimu 60 wanajitolea kwenye shule zetu.
  • Utoaji wa tuzo na zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani


MIKAKATI YA KUBORESHA TAALUMA NA UFAULU KWA SHULE ZA MSINGI MWAKA, 2022

Katika kuboresha taaluma, michezo pamoja na ufaulu kwa shule za Msingi, Halmashauri ya Mji imeandaa mikakati. Mikakati ya kitaaluma itatekelezwa chini ya kauli mbiu zifuatazo: -

“Ondoa E na D Ongeza A” kwa Shule za Msingi.

 

Mikakati hiyo ya kitaaluma na ya michezo ni pamoja na: -

  1. Kuimarisha USIMAMIZI na UFUATILIAJI ngazi ya Kata na Shule ili kuinua taaluma na kuongeza ufaulu kwa shule za msingi na sekondari na kuchukuwa HATUA STAHIKI KWA   YEYOTE atakayeshindwa kuwajibika kikamilifu.
  2. Kuongeza mazoezi kwa madarasa ya mitihani
  3.  Kudhibiti utoro wa walimu shuleni na madarasani na Walimu Wakuu kupokea taarifa za utendaji wa walimu wa kila siku.
  4. Waratibu Elimu Kata kuwasilisha taarifa ya ufuatiliaji na   usimamizi kila mwezi ili kupima utendaji wao, hatua wanazochukuwa katika kuimarisha utendaji wa walimu
  5. Kuimarisha ufuatiliaji na tathmini shuleni
  6. Kuanzisha program ya mafunzo kazini somo la ENGLISH LANGUAGE kwa walimu wa shule za msingi. Walimu mahiri wa shule za msingi na walimu wa shule za sekondari watatumika. Lengo ni kuongeza umahiri wa walimu wa shule za msingi kufundisha somo hilo ambalo kwasasa linafanywa vibaya. 
  7. Kuimarisha usimamizi wa mitihani katika ngazi zote na hasa shule za msingi ili 
  8. Kudhibiti udanganyifu wa aina zote.
  9. Kuhakikisha shule za msingi zenye upungufu mkubwa wa walimu zinatafuta walimu wa kujitolea wakiwemo vijana waliomaliza Ualimu ambao hawajaajiriwa na waliomaliza na KUFAULU Kidato cha Nne kwenye maeneo yao.
  10. Kutowasajili Darasa la Saba wanafunzi wa Darasa la Sita wasiojua KKK na badala yake kuwaombea KURUDIA Darasa la Sita.
  11. Kuimarisha maandalizi na uendeshaji wa MITIHANI YA UTAMILIFU ili iwaandae vema wanafunzi na kutoa picha halisi kabla ya kufanya mitihani yao ya Kitaifa.     
  12. Kuzifanyia UKAGUZI MAALUM shule zote zinazoshuka ufaulu kuanzia asilimia 10 katika mitihani ya kitaifa ili kubaini sababu za kufanya vibaya na kuchukuwa HATUA STAHIKI.
  13. Kuimarisha na kuboresha makambi kwa Darasa la Saba ili kuwaandaa kikamilifu kwa ajili ya mitihani inayowakabili. 



Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA VIONGOZI March 14, 2023
  • UTEUZI WA VIONGOZI March 15, 2023
  • UTEUZI NA KUBADILISHIWA VITUO KWA MAKATIBU TAWALA March 16, 2023
  • TAARIFA YA MAKUSANYO YA MAPATO KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2022/23 October 07, 2022
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • KUFIKA MWAKA 2025 TUNATAKA UNYWAJI WA MAZIWA TUNDUMA UFIKE 60% _MWALUKASA

    March 15, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 14, 2023
  • SIRI NDIO UHAI WA SERIKALI, EPUKENI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA TAARIFA ZA SERIKALI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • SITEGEMEI PIKIPIKI HIZI MWENDENAZO BAR _ DC LULANDALA

    March 11, 2023
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 752 807 767

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa