• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

Imewekwa : May 30th, 2025

Na Benton Nollo, TTC Sakania, DR Congo

Katibu Tawala Wilaya ya Momba, Frank Nkinda amesema ziara ya Viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Mji Tunduma kutembelea mradi mkubwa wa uwekezaji wa Bandari Kavu katika eneo la mpaka la Sakania hadi Mokambo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DR Congo na Nchi ya Zambia, ina manufaa makubwa kwa Mji wa Tunduma na taifa kwa ujumla.

Nkinda ameyasema hayo wakati wa ziara hiyo iliyofanyika tarehe 30 Mei 2025 ambapo viongozi hao walitembelea katika eneo hilo baada ya kupata mwaliko wa Kampuni ya TAZACO Investment Ltd ya jijini Dar es Salaam ili kwenda kujifunza namna ya uendeshaji wa bandari kavu na kupata uzoefu wa shughuli hizo ambapo katika eneo hilo zinasimamiwa na Kampuni ya Jiayou International Logistics Co. Ltd.

"Kwa kweli mradi huu unapendeza na unatija kubwa kwa wenzetu...kampuni hii ndiyo ambayo tunatarajia ije kwetu Tunduma kwa ajili ya uwekezaji na kutuboreshea eneo letu na kupunguza msongamano wa malori". Amesema Nkinda.

Kwa upande wake Makamu Meneja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Jiayou International Logistics Co. Ltd., Li Yong Qiang amesema atafurahi kuona Serikali ya Tanzania kupitia Halmashauri ya Mji Tunduma inatekeleza mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu katika eneo la Mpemba ili kupunguza msongamano wa malori uliopo sasa na kuinua uchumi wa eneo hilo na taifa kwa ujumla kwa kuwa ndiyo Lango Kuu ya SADC.

Viongozi hao wamejifunza namna Serikali ya DR Congo ilivyoingia mkataba wa makubariano ya ukarabati wa sehemu ya kipande cha barabara kwa hadhi ya kimataifa cha Kasumbalesa - Sakania chenye Vituo vya Ushuru wa Barabara (Road Tolls) vinne pamoja na Bandari Kavu mbili za Sakania na Mokambo ambapo gharama za uwekezaji wa mradi huo ni Dola za Kimarekani milioni 229 ($229 million).

Bandari Kavu ya Sakania yenye ukubwa wa hekta 144, yamejengwa majengo makubwa mawili likiwemo la Kituo Jumuishi pamoja na maegesho ya malori huku barabara iliyokarabatiwa kwa kiwango cha lami kwa hadhi ya kimataifa ina urefu wa kilomita 145 hadi Kasumbalesa ambapo 'Road Toll' ya kwanza iliyopo Kawimba ipo umbali wa kilomita 5, ya pili ya Kabembe ipo kilomita 72, ya tatu ya Tonkoshi ipo kilomita 85 na ya nne ya Lukangaba ipo umbali wa kilomita 138 kutoka Kasumbalesa kuelekea mpaka wa Sakania. Aidha, Bandari Kavu ya Mokambo nayo ina ukubwa wa hekta 20.

Mradi huo ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo tarehe 03 Oktoba 2023.

Matukio katika Picha:

Viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Mji Tunduma wakiwasili eneo la Bandari Kavu katika eneo la mpaka la Sakania kati Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DR Congo na Zambia tarehe 30 Mei 2025 ambapo viongozi hao walitembelea katika eneo hilo baada ya kupata mwaliko wa Kampuni ya TAZACO Investment Ltd ya jijini Dar es Salaam ili kwenda kujifunza namna ya uendeshaji wa bandari kavu na kupata uzoefu wa shughuli hizo ambapo katika eneo hilo zinasimamiwa na Kampuni ya Jiayou International Logistics Co. Ltd.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jiayou International Logistics Co. Ltd., Mackhy Melesi akiwasilisha wasilisho la namna mradi mkubwa wa uwekezaji wa Bandari Kavu katika eneo la mpaka la Sakania hadi Mokambo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DR Congo na Nchi ya Zambia, ulivyotekelezwa.

Makamu Meneja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Jiayou International Logistics Co. Ltd., Li Yong Qiang akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya viongozi hao walipotembelea kujionea namna mradi mkubwa wa uwekezaji wa Bandari Kavu katika eneo la mpaka la Sakania hadi Mokambo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DR Congo na Nchi ya Zambia, ulivyotekelezwa.


(Picha zote na Benton Nollo, TTC).


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa