• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

Imewekwa : June 2nd, 2025

Na Benton Nollo, TTC

Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya Halmashauri ya Mji Tunduma yameanza rasmi tarehe 02 Juni 2025 katika viwanja vya michezo vilivyopo Shule ya Sekondari Mpemba.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo, Valentine Christopher Mkomwa amesema maandalizi yamefanyika vizuri na yanajumuisha shule zote za sekondari.

“Halmashauri yetu katika Shule ya Sekondari JK Nyerere ni Kitalu kwa Wanafunzi wa Mpira wa Miguu na wanafunzi wote 20 nao watashiriki mashindano haya.” Amesema Mkomwa.

Kwa upande wake, Mwalimu wa Michezo Halmashauri ya Mji Tunduma, Daniel Mombo ametaja michezo ambayo Halmashauri ya Mji Tunduma inashiriki ni mpira wa miguu Wavulana na Wasichana, Mpira wa Kikapu Wavulana na Wasichana, mpira wa mikono Wavulana na Wasichana, riadha na mpira wa pete.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru Mkurugenzi wetu wa Halamashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo kwa kazi nzuri anayoifanya hasa katika idara ya michezo, tumeona anavyojitoa kuwezesha Wanafunzi ambao wanashiriki michezo hii ya UMISSETA mpaka ngazi ya taifa…kwa kweli amekuwa bega kwa bega na sisi.” Amesema Mwalimu Mombo.

Naye, Mwalimu Lea Godwin ambaye pia ni Mwalimu wa Michezo amesema maandalizi kwa timu zote yapo vizuri na watoto wana utimamu na utayari wa kushiriki michezo mbalimbali katika mashindano hayo.

Silas Tumaini Masodas ni Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Uwanjani yeye ni kepteni wa Timu ya Mpira wa Miguu Kanda B ambapo amesema maandalizi yote yamekamilika na kilichobaki ni wao kama wachezaji kutimiza wajibu wao ili kuleta ushindi kwa Halmashauri yao.

“Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuchaguliwa kuwa Kepteni kwenye Zone (Kanda) yangu…nawaahidi Zone yangu tutafanya vizuri, maandalizi yote yameenda vizuri, benchi la ufundi, walimu wetu wote, kwa asilimia 90 kila kitu kipi sawa, imebaki kwetu maana maelekezo yote tumepewa…kwa upande wetu tumejipanga vizuri zaidi kwa kudra za Mwenyezi Mungu Inshaalah tutashinda hatutawaangusha.” Amesema Masodas.   

Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka, hivi sasa yanafanyika ili kupata timu za michezo mbalimbali zenye jumla ya Wanafunzi 140 kwa ajili ya kishiriki mashindano hayo kwa ngazi ya mkoa hivi karibuni.

Matukio katika Picha:

(Picha zote na Julius Evandino, TTC).


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa