• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Baraza Laridhia Bilioni 36.3 2024/2025

Imewekwa : February 3rd, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kauli moja limeridhia na kupitisha rasimu ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo ni shilingi bilioni 36.3.

Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayubu Mlimba kimefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mhe. Mlimba amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 13.8 ni kutokana na vyanzo vya ndani, shilingi milioni 950.3 kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji (OC), shilingi bilioni 13.2 ni mishahara na shilingi bilioni 8.2 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu na Wahisani.

Aidha, pamoja na makisio hayo pia, Baraza hilo limeridhia makisio ya matumizi ya shilingi bilioni 16.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo (shilingi bilioni 8.254 kutoka Serikali Kuu na Wahisani na shilingi bilioni 7.852 fedha za maendeleo zinazotokana na mapato ya ndani).

“Leo hii Baraza la Bajeti tumepitisha Bajeti yetu ya 2024/2025 kuwa sehemu ya mapato na matumizi ya Halmashauri yetu kwa mwaka ujao….tunatangaza kwa kauli moja kuwa tumeridhia mapendekezo haya ya bajeti.” Alisema Mh. Mlimba.

Mhe. Mlimba ameagiza watumishi wa Halmashauri kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo na kisha kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wa Tunduma.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mariam Chaurembo amelishukuru Baraza hilo kwa kuridhia shilingi billion 2.57 kwa ajili ya kukamilisha miradi viporo yote'

Matukio katika Picha:

Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Tunduma wakijadili mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024 ambapo zimeridhiwa shilingi bilioni 36.3 zitumike. 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayubu Mlimba akizungumza wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024 ambapo zimeridhiwa shilingi bilioni 36.3 zitumike. 

Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Tunduma wakizungumza wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024 ambapo zimeridhiwa shilingi bilioni 36.3 zitumike. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo akizungumza wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024 ambapo zimeridhiwa shilingi bilioni 36.3 zitumike. 

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba, wakiwa katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024 ambapo zimeridhiwa shilingi bilioni 36.3 zitumike. 

Baadhi ya Viongozi, Wakuu wa Divisheni na Vitengo na Watendaji wa Kata wakiwa katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 03 Februari 2024 ambapo zimeridhiwa shilingi bilioni 36.3 zitumike. 


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa