• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

BILIONI 1.5 KUTUMIKA KUJENGA SOKO LA KISASA LA KUUZIA SAMAKI NA DAGAA TUNDUMA

Imewekwa : February 11th, 2023

Na William Maganga,Tunduma

Tunduma: Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha fedha Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga soko la kisasa la kuuzia samaki na dagaa ndani ya Mji wa Tunduma ili kuongeza mapato na kuokoa upotevu wa mapato uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wafanya biashara waliokuwa wakisafirisha bidhaa hizo kwenda nchi za SADC pasipo kulipia.

Akizungumza leo tarehe 10/2/2023 mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Ayoub Mlimba alisema kwa muda mrefu walikuwa wakikosa mapato kutokana na watu wengi kutunza samaki kwenye nyumba za watu zilizopo pembezoni mwa mpaka wa Tunduma na Zambia.

 Alisema uwepo wa stoo hizo uliwafanya wafanyabiashara wasio wazalendo kusafirisha shehena za Samaki na Dagaa hata usiku wa manane huku maafisa wa ukusanyaji ushuru wakishindwa kukusanya ushuru hali iliyoikosesha mapato halmashauri na hata idara husika kushindwa kukusanya takwimu sahihi.

‘’Leo tupo hapa tunasaini mkataba kwa kulipa fidia kwa wamiliki wa eneo ambapo tunatarajia kujenga Soko hilo ambalo lina ukubwa wa Hekari 3.3, kwa makubaliano ya halmashauri kuilipa familia hii Milioni 30 pamoja na viwanja 2 vyenye urefu wa mita za mraba 600 kila kimoja’’alisema Mhe. Mlimba.

Aidha Mhe. Mlimba alisema katika kipindi cha utawala wake mikataba yote itakuwa ikisainiwa eneo husika badala ya ofisini ili kuwepo na uwazi na kila mwenye malalamiko aweze kutoa ili kukwepa migogoro isiyokuwa ya lazima pia kuwafanya wananchi kushiriki tangu mwanzo wa mradi hadi kukamilika kwake.

Afisa Uvuvi wa halmashauri ya mji huo Bwana Elivathan Silwimba alisema kuwa Serikali imefanya jambo la muhimu kwani ujenzi wa soko hilo eneo hilo la Chapwa litasaidia kuzuia utoroshwaji wa samaki, hasa kutokana na jinsi mpaka ulivyokuwa wazi masaa 24 huku stoo za dagaa ziko kwenye nyumba za watu.

Aliongeza kuwa sheria za uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 inakataza kusafirisha mazao ya uvuvi baada ya saa 12 jioni, kwani kusafirisha muda huo hakuna anayechukua takwimu.

“Kwa kipindi hiki Halmashauri ya Mji Tunduma inasafirisha Mazao ya Samaki ni gunia 2000 na dagaa ni gunia 5000 kwa mwaka, nina Imani ujenzi wa soko hili takwimu hizi zitaongezeka maradufu” alisisitiza Silwimba

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Ndugu Philemon Magesa alisema serikali imekuwa ikiwapatia fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na kwa ujio wa Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo kutaongeza chachu ya kiuchumi kwa serikali na mtu mmoja mmoja.

Alisema mradi utakapokamilika wataweza kujenga barabara zitakazofunguka na kulifanya eneo hilo la Chapwa kushangamka kiuchumi kwani watu wengi watafungua biashara maeneo hayo wakiwemo mama lishe hivyo wanatarajia kuukamilisha mradi huo kwa wakati ili kuleta manufaa kwa wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa