• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Bilioni 343.4 Zatekeleza Miradi ya Maendeleo Songwe, Kati ya Hizo Bilioni 38 Zanufaisha Tunduma

Imewekwa : January 30th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Mkoa wa Songwe katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Desemba 2023 umepokea shilingi bilioni 343.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha maisha ya Watanzania.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael wakati wa mkutano wake na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024.

Lengo la Mkutano huo ulioratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO kupitia Programu ya Tumewasikia, Tumewafikia chini ya Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, ni kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka mitatu mkoani Songwe.

Dkt. Michael amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Songwe umepokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, biashara, maji, umeme, miundombinu ya barabara, kilimo, uvuvi, viwanda na biashara.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa hatua zilizochukuliwa na Rais Samia zimeleta mabadiliko mengi na chanya katika Mkoa wa Songwe ambapo kwa dhati zinalenga kuboresha maisha ya Wananchi kwa kuleta maendeleo.

Akiwasilisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu ya Halmashauri hiyo, Belton Garigo amesema Halmashauri ya Mji Tunduma imepokea shilingi bilioni 38 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Garigo alisema kwa upande Elimu Msingi kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita Halmashauri ya Mji Tunduma ilikuwa na Shule za Msingi 25 wakati kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri hiyo ina shule za msingi 52, vyumba vya madarasa vilikuwa 350 wakati kwa kipindi hicho tayari kuna vyumba vya madarasa 550, walimu waliokuwepo ni 400 wakati mpaka Desemba 2023 kuna walimu 510.

Garigo aliongeza kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani Machi 2021, Halmashauri ya Mji Tunduma ilikuwa na matundu ya vyoo 610 wakati mpaka Desemba 2023 Halmashauri ina matundu ya vyoo 983, madawati yalikuwa 4,705 wakati mpaka kipindi hicho kuna madawati 9,568 na kiwango cha ufaulu Darasa la Saba mpaka kufikia asilimia 94.1 mwaka 2023 kutoka asilimia 78 mwaka 2021.

Kwa upande wa Elimu Sekondari, Garigo alisema mwezi Machi 2021 kulikuwa na Shule za Sekondari za Serikali 11 ambapo mpaka Desemba 2023 kuna Shule za Sekondari za Serikali 16 wakati kwa Kidato cha Tano na Sita zimefikia shule 4 kutoka shule 2 mwaka 2021.

Garigo alisema mwaka 2021 hakukuwa na shule za sekondari za bweni lakini mpaka Desemba 2023 yamejengwa mabweni ya Wavulana na Wasichana katika Shule ya Sekondari Namole na Dkt. Samia SH. Alisema mwaka 2021 kulikuwa na nyumba za Walimu 11 wakati mpaka kufikia Desemba 2023 kuna nyumba za walimu 20, idadi ya Walimu imeongezeka kutoka 238 mwaka 2021 hadi 290 mwaka 2023. Alisema mwaka 2021 kulikuwa na wanafunzi 8,888 wakati mpaka Desemba 2023 kuna wanafunzi 11,400, huku kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne kimeongezeka na kufikia asilimia 98.4 kutoka asilimia 95.4 mwaka 2021.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa Habari, ujenzi wa shule mpya na ongezeko la vyumba vya madarasa vimesaidia kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kufuata huduma ya elimu maeneo ya mbali pia imepunguza mlundikano na utoro wa rejareja...ongezeko la Waalimu pamoja na uboreshaji wa miundombinu mingine ya shule imefanya kiwango cha ufaulu kuongezeka.” Alisema Garigo.

Katika Sekta ya Afya, Garigo alisema vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 5 mwaka 2021 hadi vifo 3 mwaka 2023 huku vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 27 mwaka 2021 hadi vifo 26 mwaka 2023. Kwa upande wa Zahanati zimeongezeka kutoka zahanati 4 mwaka 2021 hadi zahanati 8 mwaka 2023, Vituo vya Afya vimeongezeka kutoka kituo cha afya kimoja mwaka 2021 hadi vituo vya afya 6 mwaka 2023. Alisema mwaka 2021 hakukuwa na Hospitali ya Serikali lakini hadi kufikia mwaka 2023 kuna Hospitali moja ya Mji Tunduma.

Garigo alisema huduma za afya zimesaidia kupunguza vifo visivyo vya lazima kwani kuongezeka kwa miundombinu ya Afya kumepunguza kero ya Wananchi kutembea muda mrefu kutafuta huduma. Aidha, kiwango cha upatikanaji wa dawa kimeongezeka kutoka asilimia 86 na kufikia asilimia 96 hali inayopelekea wagonjwa wengi kuepukana na hali ya kukosa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.  

Sekta ya Kilimo Garigo alisema idadi ya Maafisa ugani kilimo na mifugo walikuwepo 26 mwaka 2021 na hadi Desemba 2023 kuna Maafisa ugani kilimo na mifugo 28. Kwa upande wa vitendea kazi mwaka 2021 kulikuwa na pikipiki moja lakini mpaka kufikia Desemba 2023 Halmashauri ina pikipiki 32 huku utolewaji wa mbolea ya Ruzuku mwaka 2021 ulikuwa ni kwa baadhi ya wakulima lakini mpaka Desemba 2023 Wakulima 11,800 wamepatiwa mbolea ya ruzuku.

Kadhalika, kwa sekta ya viwanda mwaka 2021 kulikuwa na viwanda vidogo vipatavyo 439 ambavyo ni vya kusindika mazao ya mpunga, mahindi, alizeti useremala, kuchomelea na ushonaji lakini mpaka kufikia Desemba 2023 Halmashauri ina viwanda vidogo 451 ambapo kuna ongezeko la idadi ya viwanda 102 ambavyo vimezalisha ajira mpya kwa vijana wapatao 306.

Kwa upande wa uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Desemba 2023 shilingi bilioni 3.8 zilitengwa kwa ajili ya mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya ujasiriamali ya wanawake, vijana na walemavu kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani na marejesho. Garigo alisema kwa kipindi hicho jumla ya shilingi bilioni 2.8 zimekopeshwa kwa vikundi 178 (Wanawake vikundi 75, Vijana vikundi 69 na Walemavu 34).

Amefafanua kuwa mwaka 2021 idadi ya vikundi vya Wanawake,Vijana na wenye ulemavu ilikuwa ya wastani kujitokeza kukopa mikopo ambapo kulikuwa na vikundi 167, kati yake vikundi vya wanawake 99, vikundi vya vijana 54 na Watu Wenye Ulemavu 14 vilijitokeza kuomba mikopo na kufanikiwa kukopeshwa ilhali mpaka kufikia Desemba 2023 ongezeko ni kubwa la uundaji wa vikundi kufikia  vikundi 336 kati yake vikundi vya wanawake ni 171, vikundi vya vijana ni 120 na Watu Wenye Ulemavu ni 45 hii ni kutona na kuongezeka kwa hamasa juu ya utoaji wa mikopo katika Halmashauri kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Garigo alisema utoaji wa mikopo bila riba umesaidia   wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kujiinua kiuchumi, kukuza vipato vyao na imesaidia kutoa ajira kwa vijana ambao hawakuwa na kazi za kufanya mfano utoaji wa pikipiki kwa vijana na vijana wanaojishughulisha na shughuli za kitaalamu hasa upimaji wa ardhi.

Matukio katika Picha:

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael akizungumza wakati wa mkutano wake na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024 kwa lengo la kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Desemba 2023.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda akizungumza awali wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024 kwa lengo la kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Desemba 2023.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO,  Rodney Thadeus akizungumza na kufafanua dhana ya Tumewasikia, Tumewafikia na umuhimu wa kutangaza miradi na shughuli za Serikali kwa Wananchi,  wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024 kwa lengo la kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Desemba 2023.

Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Mji Tunduma, Belton Garigo kwa niaba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo akiwasilisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu (Machi 221 hadi Desemba 2023) wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024 kwa lengo la kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Desemba 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael (katikati), Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo na Viongozi mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu yaliyokuwa yakiwasilishwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi akifuatilia kwa makini mawasilisho ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu yaliyokuwa yakiwasilishwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Songwe wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024.

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Songwe wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu yaliyokuwa yakiwasilishwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024. Kuanzia kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongozi, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda, wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya Mbozi, Mhe. Esther Mahawe na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Farida Mgomi.

Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Songwe wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu (2021 hadi 2023) wakati wa Mkutano wa kiongozi huyo na Wakurugenzi hao kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024. Kuanzia kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Belton Garigo, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Nuru Waziri Kindamba, wa tatu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya WIlaya ya Momba, Fabian Manoza Said, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde na wa piku kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, CPA. Cecilia Donath Kavishe.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari mara baada ya Mkutano wa kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu katika Mkoa wa Songwe ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Francis Michael na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus (kulia) wakizungumza mara baada ya Mkutano wa kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu katika Mkoa wa Songwe ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Francis Michael na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kwa Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mlowo tarehe 30 Januari 2024. (Picha zote na Benton Nollo, TTC).


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa