• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DC Mgomi Mgeni Rasmi Mahafali ya Kwanza Dkt. Samia SH

Imewekwa : April 25th, 2025

Atwiya Mohamed na Silvesta Mtafya, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Farida Mgomi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe.  Daniel Chongolo, amekuwa mgeni rasmi wa kwanza katika Mahafali ya Kwanza ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia SH yaliyofanyika shuleni hapo tarehe 25 Aprili 2025.

Mhe. Mgomi amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Momba, Halmashauri ya Mji Tunduma, Walimu pamoja na Wazazi kwa maandalizi mazuri ya mahafali hayo ya kwanza na kihistoria.

"Niwatie moyo katika kipindi hiki cha maandalizi yenu ya mwisho kuelekea mtihani wenu wa taifa...mtakapokuwa katika chumba cha mtihani kuweni watulivu katika kujibu maswali, kubwa na muhimu ni kujiamini na sisi tunawaamini kwani mnao uwezo mkubwa wa kufanya vizuri." Amesema Mhe. Mgomi na kuongeza;

"Mkoa wa Songwe unaona fahari kubwa kuwa na ninyi hasa ikizingatiwa ninyi ndiyo zao la kwanza la Shule ya Wasichana katika Mkoa wetu wa Songwe...matarajio tuliyonayo kwenu ni makubwa katika matokeo na hata baada ya matokeo ili mje kulitumikia taifa letu."

Mhe. Mgomi amesisitiza kuwa Mkoa unatarajia kubebwa kwa matokeo mazuri yatakayotokana na wahitimu hao.

"Niwaombe mkawe mabalozi wazuri wa Serikali na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye jina lake limetumika kama jina la Shule yenu...msituangushe." Amesisitiza Mhe. Mgomi na kuongeza;

"Mmekuwa hapa kama timu moja na mmeishi kwa kushirikiana lakini kila mmoja ana ndoto yake na matamanio ya kesho yake, nendeni mkaziishi ndoto zenu mlizo nazo na Tanzania bora ya kesho inawahitaji na taifa linawategemea."

"Niwatakie kheri na baraka Wahitimu wote katika Mtihani wenu wa taifa wa Kidato cha Sita, lakini pia niwatakie maisha mema hata baada ya kuhitimu masomo yenu." Amesema Mhe. Mgomi.

Akizungumza awali Mkuu wa Shule hiyo, Anna Salutary Mushi amesema mpaka sasa Shule hiyo ina Walimu 22 na Wanafunzi 614 wa kidato cha Kwanza, Pili, Tano na Sita ambapo kati yao wanaohitimu ni 181.

 Mushi amesema kuwa mpaka kukamilika kwa Shule hiyo itachukua Wanafunzi 920 ambapo Tahasusi zilizopo ni PCB, PCM, EBG, HGE, HKL na HGK.

Matukio katika Picha:

(Picha zote na Julius Evandino, TTC).

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa