• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

DCC Yaridhia Bilioni 36.3 Zitumike Tunduma

Imewekwa : January 31st, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Momba – DCC imeridhia na kupitisha rasimu ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya shilingi bilioni 36.3 yatumike na Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi kimefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mhe. Kihongosi alisema baada ya Bajeti hiyo kuidhinishwa na Bunge, Halmashauri ya Mji Tunduma ihakikishe kuwa bajeti hiyo inaheshimiwa na inatekelezwa kama ilivyoidhinishwa.

“Niwaombe sana Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wetu tujifunze kuheshimu fedha za umma na kusimamia utekelezaji wa miradi kama mipango inavyotuelekeza ili thamani ya fedha katika miradi husika ionekane na iwanufaishe na kuleta tija kwa Wananchi. Alisema Mhe. Kihongosi.

Awali akiwasilisha mapendekezo ya Makadirio ya Makusanyo ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Belton Garigo alifafanua kuwa kati ya shilingi bilioni 36.3 zinazopendekezwa, shilingi bilioni 13.8 ni kutokana na vyanzo vya ndani, shilingi milioni 950.3 kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji (OC), shilingi bilioni 13.2 ni mishahara na shilingi bilioni 8.2 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu na Wahisani.

Aidha, pamoja na makisio hayo pia, Kamati hiyo imeridhia makisio ya matumizi ya shilingi bilioni 16.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo (shilingi bilioni 8.254 kutoka Serikali Kuu na Wahisani na shilingi bilioni 7.852 fedha za maendeleo zinazotokana na mapato ya ndani).

Kikao hicho maalum kimehudhuriwa na Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Momba kwa lengo la kupitisha mapendekezo ya makisio ya Mipango na Bajeti kwa Halmashauri hizo kwa mwaka 2024/2025.


Matukio katika Picha:

Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya WiIaya ya Momba - DCC ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Kenani Kihongosi akizungumza wakati wa kikao maalum cha Kamati hiyo kilichoketi kwa ajili ya kujadili na kuridhia Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri zote mbili (Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya ya Momba) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024.

Viongozi na Wajumbe Kamati ya Ulinzi na Usalama WiIaya ya Momba wakisoma kwa makini kabrasha la rasimu ya mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya hiyo - DCC  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Ayubu Mlimba akizungumza mara baada ya Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kuwasilishwa kwenye kikao Maalum cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Momba - DCC kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024.

Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Mji Tunduma, Belton Garigo akiwasilisha Mapendekezo na Mpango wa Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye kikao Maalum cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Momba - DCC kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Ayubu Mlimba (kushoto) akiteta jambo na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mwanaisham Nassor (kulia) wakati wa kikao Maalum cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Momba - DCC kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024  kwa ajili ya kujadili Mapendekezo na Mpango wa Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Wakuu wa Divisheni na Vitengo wakifuatilia uwasilishaji wa mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya hiyo - DCC  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete tarehe 31 Januari 2024.





Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa