• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Jamii Tunduma Yatakiwa Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Imewekwa : December 5th, 2023

Na Benton Nollo, Tunduma TC

Jamii katika Mji wa Tunduma imetakiwa kujiepusha na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwani vina madhara makubwa katika ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Mwanaisham Nassor (pichani) tarehe 05 Disemba 2023 alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake kuhusu Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba.

Nassor amesema Divisheni hiyo kwa kushirikiana na Wadau Mbalimbali wa Maendeleo inaratibu Kampeni hiyo yenye lengo la kuongeza ushawishi, kujenga uwezo wa pamoja na kuunganisha nguvu za asasi za kijamii katika kuhamasisha, kuelimisha, kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.

Amefafanua kuwa Kampeni hiyo ambayo kitaifa imezinduliwa tarehe 25 Novemba 2023 mkoani Dar es Salaam inafanyika katika ngazi zote kuanzia mtaa, kata na Halamshauri ambapo Kaulimbiu ni “Wekeza: Kuzuia Ukatili wa Kijinsia.”

Nassor amesema kaulimbiu hiyo inalenga kusisitiza jamii kuwekeza zaidi katika kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana ikiwa ni kundi ambalo linapitia changamoto zaidi za vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Wanawake na Wasichana ndiyo kundi linalopitia changamoto nyingi kutokana na mgawanyo wa majukumu katika familia, uwezo mdogo wa kipato, elimu na ujuzi duni, mila na desturi kandamizi na ukubwa wa wategemezi kwenye kaya, hivyo ni muhimu sana kuimarisha ustawi wa maendeleo ya wanawake na wasichana ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.” Amesema Nassor.

Nassor amesema Kampeni hiyo inaongozwa na sera za kijumla na sera za kisekta ambapo amefafanua kuwa sera za kijumla ni pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na sera za kisekta ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) wakati maazimio ni pamoja na yale ya Ulingo wa eijing kwa miaka 27.

Ameyataja maazimio mengine kuwa ni Ajenda 2030 ya Malengo Endelevu hususan lengo Namba 5 linalohusu Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi na Ajenda ya Maendeleo ya Bara la Afrika 2063.

Nassor amesema maazimio mengine yanayotoa uhalali wa kuadhimisha Kampeni hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Sheria ya Urithi, Mirathi ya Wosia, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na Sheria nyingine.

Aidha, Nassor amesema kwa Tanzania kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika, vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikiongezeka kwa kasi kubwa ambapo kwa upande wa watoto ni watoto 5 hadi 10 hufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali.

“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kushirikiana na Halmashauri ya Mji Tunduma katika Kampeni hii. Wadau hao ni Redio Tunduma NLC FM 92.1, Kikundi cha Watoa Huduma na Waelimisha Rika Songwe (KIWAWASO), Shirika Lisilo la Kiserikali la Wasaidizi wa Kisgheria – GSRO na Dawati la Jinsia la Polisi Wilaya ya Momba ambao tumeshirikiana kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika shule za msingi 14 ambazo ni Mizani, Haisoja, Fura, Kigamboni, Chapwa ‘A’, Ushindi, Mpakani, Mlimani, Mwaka, Tunduma, Sogea, Makambini, Maporomoko, Katete na Mpemba.’ Amesema Nassor na kuongeza;

“Maeneo mengine ni Soko la Machinga Tunduma, Soko la Mpemba, Kituo Kikuu cha Mabasi Tunduma kilichopo Mpemba, Vituo vya Daladala Chapwa, Sogea na Kisimani pamoja na Vikundi 12 vya Wauza Samaki na Dagaa eneo la Majengo.”

Kadhalika, amefafanua kuwa ukatili huo unajitokeza katika sura mbalimbali kama vile vipigo, ukeketaji, ubakaji, mauaji ya wanawake na watoto wa kike, kurithi wajane, mimba za utotoni na ukatili wa nyumbani. Ukatili una madhara kwa Wanawake kwani huathiri afya zao kimwili na kisaikolojia na hivyo kusababisha kudidimia kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

 Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ni Kampeni kabambe ya kimataifa inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha Wanawake katika Uongozi (Women’s Global Leadership) tangu mwaka 1991. Aidha, Kampeni hiyo ilitokana na mauaji ya kinyama ya Wanawake wa Mirabelle yaliyotokea nchini Dominica mwaka 1960.


Matukio Katika Picha:

Wataalam wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa jamii kupitia Kituo cha Redio cha Tunduma NLC FM 92.1 kilichopo mjini Tunduma ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwaka tarehe 26 Novemba 2023 ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Wataalam wa Ustawi wa Jamii na Wasaidizi wa Kisheria Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makambini tarehe 27 Novemba 2023 ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpakani tarehe 28 Novemba 2023 ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Wataalam wa Ustawi wa Jamii na Wasaidizi wa Kisheria Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Fura tarehe 27 Novemba 2023 ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Vikundi vya Wanawake tarehe 30 Novemba 2023 ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tunduma kwa nyakati tofauti wakitoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wajasiriamali wa Soko la Machinga Kata ya Majengo Tunduma mjini tarehe 5 Desemba 2023 ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. (Picha zote na Julius Evandino wa TTC).

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa