• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Kakusanyeni Mapato: Chaurembo

Imewekwa : February 13th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo amewaagiza Watendaji wa Kata na Mitaa kukusanya mapato ya Halmashauri na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Chaurembo ametoa agizo hilo wakati wa kikao kazi na Watendaji wa Kata 15 na Watendaji wa Mitaa yote 71 ya Halmashauri hiyo, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 13 Februari 2024.

Chaurembo ameeleza kwamba katika kuhakikisha kuwa zoezi la ukusanyanyi Mapato linafanyika ipasavyo, Halmashauri ya Mji Tunduma inapaswa kuwa na Nanzidata ya Wafanyabiashara wote katika kila mtaa hivyo aliwaagiza Watendaji hao kuwa mpaka kufikia tarehe 29 Feruari 2024 wawe wamesilisha Kanzidata ya Wafanyabiashara ndani ya Kata na Mitaa yao.

“Watendaji ninyi ndiyo nguzo yangu ya kwanza kuliko mtu mwingine yeyote katika ukusanyaji wa mapato…hivyo mnao wajubu mkubwa kuhakikisha kuwa mapato yanakusanywa ipasavyo, kwa katika kila tunachokikusanya, asilimia 60 inarudi kuwahudumia Wananchi katika sekta mbalimbali.” Amesema.

Chaurembo amewataka Watendaji hao kuhakikisha kuwa mapato yote yanakusanywa kwa kutumia PoS na fedha zote zinazokusanywa kupelejkwa Benki kwa wakati na si vinginevyo.

Aidha, katika hatua nyingine Chaurembo amewataka Watendaji hao kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kuitembelea miradi hiyo mara kwa mara ili kujionea hatua zote za utekelezaji.

“Nikija kwenye mradi nataka kuona ushiriki wako katika mradi huo na nitakagua kitabu cha eneo la mradi na kitabu cha wageni…nataka nikute vitabu vina saini zenu, umebanwa sana basi angalau kwa wiki uende mara mbili kwenye mradi.” Amesema Chaurembo na kuongeza;

“Tumeagiza pikipiki kadhaa kwa ajili ya Watendaji wa Kata ili kuwarahisishia zoezi la kutembelea na kufuatilia miradi…lakini wakati tunasubiri pikipiki hizo mnatakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yenu kama kawaida.”

Pamoja na mambo mengine, Chaurembo amewakumbusha Watendaji hao kutembelea Vituo vya Afya, Zahanati na Shule ili kubaini iwapo kuna changamoto zozote zinazowakabili Wananchi ili waweze kuzitatua kwa wakati.

Mambo mengine aliyoyasisitiza Mkurugenzi huyo ni pamoja na Watendaji hao kutatua migogoro ya ardhi, kufuatilia urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 na kukaa kwenye vituo vyao vya kazi ili wawahudumie Wananchi ipasavyo bila kuomba chochote wala upendeleo.

Aidha, Chaurembo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia fedha za miradi ya maendeleo Halmashauri hiyo kwani kwa kufanya hivyo anatatua changamoto za Wananchi.

Halmashauri ya Mji Tunduma, pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea, pia katika kipindi cha Mwezi Januari 2024 imepokea shilingi bilioni 2.7 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya afya na elimu.

Matukio katika Picha:

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo akizungumza wakati wa kikao kazi na Watendaji wa Kata na Mitaa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 13 Februari 2024.

Baadhi ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo wakizungumza wakati wa kikao kazi na Watendaji wa Kata na Mitaa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 13 Februari 2024. Kikao hicho kiliongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo.

Baadhi ya Watendaji wa Kata wakizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 13 Februari 2024. Kikao hicho kiliongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo na kuwahusisha Watendaji wa Kata na Mitaa wote katikas Halmashauri hiyo.

Baadhi ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo na Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo wakati wa kikao kazi na Watendaji wa Kata na Mitaa yote kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 13 Februari 2024. 


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa