Halmashauri ya Mji Tunduma imeanza vikao vya kujiandaa kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa watendaji wa Kata na mitaa yote ya Halmashauri ya Mji Tunduma
Akiongea katika kikao kazi hicho Mratibu wa Sensa ya watu na makazi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Bi. Angela Francis Njaritta amewaeleza watendaji wa kata na mitaa juu ya umuhimu mkubwa wa Sensa na Faida zake
Katika wasilisho lake Bi. Angela aliwaambia washiriki kuwa “Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kama zilivyo sensa nyingine zilizotangulia itatoa majawabu katika mambo ya msingi yanayohusu watu kiafya, kielimu, kijamii, kimazingira na kiuchumi”
Upimaji wa mipango mbalimbali ya Serikali hutegemea taarifa zinazotokana aidha na Sensa au Tafiti ambazo chimbuko lake ni Sensa ya Watu na Makazi
Pia Bi. Angela alieleza Sababu za kufanya sense katika nchi ni;
Kwanza ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351 ambayo inamuagiza Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa kushirikana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar, kufanya Sensa ya Watu na Makazi kila baada ya miaka kumi
Pili ni kukidhi matakwa ya Umoja wa Mataifa unaolekeza kila Nchi Mwanachama kupitia Ofisi za Takwimu kuhakikisha Sensa ya Watu ya Makazi inafanyika kila baada ya miaka mitano au kumi kutegemeana na Uchumi wa Nchi husika
Hivyo, nchi zote duniani ikiwemo Tanzania zinatekeleza Mpango Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Kufanya Sensa ya Watu na Makazi Duniani kwa Miaka ya 2020 ambao unatekelezwa kati ya mwaka 2015 hadi 2024
Utekelezaji wa Sensa, ni moja ya ahadi ya chama kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 Kifungu Namba 206 (i) ambacho kinaelekeza kufanyika Sensa na tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022
Aidha naye Mchumi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Bwana Agustino Ngetwa aliwaelekeza washiriki juu ya faida kuu za Sensa ya watu na makazi kama ifuatavyo;
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa