• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

MIKOPO YA BILIONI 3.6 KUIBADILISHA TUNDUMA KWA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI_ Mhe. Silinde

Imewekwa : December 28th, 2022

Mbunge wa Jimbo la Tunduma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. David Ernest Silinde amesema kuwa sasa anaiona Tunduma inayokwenda kuongozwa na watu wa aina tatu yaani Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutokana na mikopo inayotolewa na Halmashauri kipitia mapato ya Ndani

Akiongea mapema leo tarehe 28 Disemba 2022 wakati akikabidhi hundi ya Mikopo yenye thamani ya Tsh. 554,300,000/= kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Silinde amesema kuwa mapato ya Halmashauri ya Mji Tunduma yamekuwa maradufu na hii ni kutokana na udhibiti wa mianya ya ufujaji wa Mapato na kubuni vyanzo vipya vya kukusanya mapato ndani ya Mji wa Tunduma

Mhe. Silinde ameendelea kumshuruku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazoendelea kuzifanya za kuhakikisha asilimia kumi (10%) ya makusanyo ya kila Halmashauri nchini lazima itolewe mikopo kwa wananchi ili kujikwamua kiuchumi

“Mwaka huu wa fedha Halmashauri imeweza kutenga Shilingi 732,597,046.00, kwa kipindi cha Julai – Disemba 2022 Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi 1,104,300,000.00 ikiwa kiasi cha shilingi 650,000,000.00 ni mapato ya ndani na kiasi cha Shilingi 454,300,000.00 kutoka fedha za marejesho” alisema Mhe. Silinde  

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Bi. Mwanaisham Shemaghembe amesema Halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa kila pesa inayokusanywa basi 10% inatengwa kwa ajili ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu

“Nipende tu kuwasitiza kutii mikataba kwa kuzingatia vipengele vyote na kuhakikisha kuwa mmetekeleza miradi mliopanga ili kukuza kipato cha mmoja mmoja, kipato cha familia na kipato cha kikundi kwa maslahi mapana ya Halmashauri na Nchi kwa ujumla” alisisitiza Bi. Mwanaisham

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma Mhe. Ayubu Mlimba amesema kuwa Halmashauri ya Mji Tunduma kupitia Baraza la madiwani kwa kuwasaidia wananchi imeweza kutekeleza Agizo la Serikali la kutenga Asilimia 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake (4%), Vijana (4%) na watu wenye ulemavu (2%).

“Niwaombe mikopo hii ambayo mnaenda kusaini mikataba leo mrejeshe kwa wakati ili Halmashauri iendelee kuwaamini na kuendelea kuwapa mikopo Zaidi kwani mikopo ni endelevu na kila mwaka inatengwa kwa ajili ya vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu na tunataka kama ukikopa ukarejesha bila shida mkopo ujao tukupatie mara mbili ya ulichopewa sasa” alisisitiza Mhe. Mlimba

Hadi kufikia Septemba 2022 Halmashauri ya Mji Tunduma imeweza kutoa jumla ya Tsh 3,643,463,622.00 kwa vikundi vya Wanawake 178, Vijana 112, na Wenye ulemavu 42 kuanzia mwaka wa Fedha 2015/2016 hadi 2021/2022

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa