Halmashauri ya Mji Tunduma katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 iliidhinisha ujenzi wa ghorofa lenye vyumba 10 vya madarasa kwenye shule ya msingi Haisoja.
Mradi huu ulianzishwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye shule za msingi Sogea na Haisoja kwani shule hizi zina idadi kubwa sana ya wanafunzi. Mradi huu ulianza kutekelezwa rasmi kwenye shule hii mwishoni mwa mwaka 2021. Ambapo vifaa vyote vinanunuliwa na kamati ya manunuzi na ujenzi unafanywa na kampuni ya ujenzi iliyopewa dhamana inayoitwa NESHAL INVESTIMENT COMPANY LIMITED. Kwa muda ya siku 120 sawa na miezi 4.
Mradi huu hadi kukamilika unakadiliwa kutumia jumla ya Tsh. 651,128,504.21 ambapo chanzo cha fedha ni mapato ya ndani ya Halmashauri.
Manufaa ya mradi wa ujenzi wa vyuma 10 vya madarasa ambayo yanajengwa kwa ghorofa ni kuwa utasaidia sana kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa katika shule za msingi Sogea na Haisoja. Vilevile wanafunzi watasoma katika mazingira rafiki hivyo ufaulu utaongezeka. Mradi huu utahudumia idadi kubwa ya wanafunzi kwenye eneo dogo. Pia mradi huu utakuwa mradi wa mfano kwa ufanisi wa miradi mingine ya maghorofa itakayoendelea kujengwa kwenye shule zetu.
Katika utekelezaji wa mradi huu kazi ambazo zimetekelezwa mpaka sasa katika awamu ya kwanza ya msingi ni sawa na 100% ambazo kwa mujibu wa mkataba ni Pamoja na :-
Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ujenzi wa kuta na kumwaga zege kwenye nguzo.
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa