• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Msiingie Katika Vishawishi Vitakavyoharibu Ndoto Zenu: Mnzava

Imewekwa : September 4th, 2024

Na Benton Nollo, TTC 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Elliakimu Mnzavva amewataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpemba kuzingatia masomo na kuepuka vishawishi ambavyo vinaweza kuwaharibia ndoto zao.

Mnzava ameyasema hayo tarehe 04 Septemba 2024 wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya.

“Sisi tunawatakia heri kwenye masomo yenu, lakini pia mnapoendelea kujifunza masuala haya ya kuzuia na kupambana na Rushwa lakini pia Dawa za Kulevya shikeni sana masomo yenu, msiingie katika vishawishi vyovyote vile ambavyo vitaharibu ndoto zenu.” Amesema Mnzava na kuongeza;

“Msijihusishe kwa namna yoyote ile hata kujaribu kwenye matumizi ya Dawa za Kulevya…kwa sababu madhara yake ni makubwa na ndoto zenu zitakatishwa kabisa, kwa sababu utaingia kidogo kidogo baadaye unakuwa mraibu kabisa wa matumizi ya Dawa za kulevya, halafu wazazi wamekuleta hapa ili usome na walimu wanaendelea kukulea na jamii inakutegemea na Mheshimiwa Rais ameendelea kujenga miundombinu mizuri sana ya elimu ili ninyi mpate nafasi nzuri ya kujifunza lakini siyo mambo mengine.

Kiongozi huyo amesema amefarijika kuona kuwa Klabu hiyo ilizinduliwa mwaka 2010 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakati huo Dkt. Nassoro Ally Matuzya ikiwa na Wanachama 81 na mpaka sasa ina Wanachama 350 ambapo Wavulana ni 173 na Wasichana ni 177 ikiwa hai na wanaendelea kujifunza masuala ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa lakini sasa imeongezeka kipengele cha Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

“Dhamira ya Serikali ni ile ile, kwamba Klabu hizi zitaendelea kutusaidia kujenga na kutengeneza vijana wazuri ambao watakuwa wazalendo kwa taifa lao, watakaokuwa wanaendelea kuipenda haki kutoka ndani ya mioyo yao kwa sababu ni mambo ambayo watakuwa wameishi nayo kwa muda mrefu na kujifunza angali wakiwa wadogo.” Amesema Mnzava na kuongeza;

“ Ndiyo maana Klabu hizi zinaanzishwa katika ngazi zote za masomo, shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu ili kesho tupate Watumishi waadilifu wenye kupenda maslahi mapana ya taifa hili bila kujitanguliza wao wenyewe, ikiwa ni kwenye sekta binafsi ama kwenye sekta ya umma lakini hata wakiwa viongozi watakuwa wanatoa maamuzi ambayo yana maslahi mapana sana ya taifa kwa sababu wameshaelewa mapema kabisa ya kwamba rushwa ni adui wa haki na rushwa ni adui wa maendeleo lakini pia ni kosa kisheria.” Amesisitiza Mnzava.

Mnzava ameikumbusha jamii kuwa mapambano dhidi ya Rushwa si jukumu la Serikali kupitia TAKUKURU peke yake bali ni jukumu la kila Mtanzania kwa sababu athari zake zinamgusa kila mtu kwa namna tofauti tofauti.

Matukio katika Picha:

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Elliakimu Mnzava akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpemba wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya  tarehe 04 Septemba 2024 .

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Elliakimu Mnzava (kushoto) akimkabidhi Hati ya Ukaguzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya Mwenyekiti wa Klabu hiyo Shule ya Sekondari Mpemba, Sophia Bilingi (kulia) wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua Klabu hiyo  tarehe 04 Septemba 2024 .

Mwenyekiti wa Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya Shule ya Sekondari Mpemba, Sophia Bilingi  akisima taarifa ya Klabu hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Elliakimu Mnzava (hayupo pichani)  wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua Klabu hiyo  tarehe 04 Septemba 2024 .

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Elliakimu Mnzava (wa pili kulia) akipokea taarifa ya Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya Shule ya Sekondari Mpemba kutoka kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sophia Bilingi  (kushoto) wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua Klabu hiyo  tarehe 04 Septemba 2024 .

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Elias Mwandobo akizungumza awali kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Elliakimu Mnzava (hayuo pichani) ili azungumze na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpemba wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya  tarehe 04 Septemba 2024 .

(Picha zote na Julius Evandino)


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa