• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Nendeni Mkajiandikishe Muwe Sehemu ya Uamuzi wa Busara: RC Chongolo

Imewekwa : October 19th, 2024

Benton Nollo na Shadida Salum, TTC

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amewahamasisha Wananchi wa Mji wa Tunduma kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Orodha ya Wapiga Kura ili wapate sifa za kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Chongolo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Mji wa Tunduma tarehe 19 Oktoba 2024 mara baada ya kushiriki na kuhitimisha mazoezi ya mbio za mwendo wa pole na matembezi maalum yaliyoratibiwa na uongozi wa mkoa huo maarufu kama Songwe Route Match 2024.

Akizungumza katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma yalipofanyika mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali, Chongolo ameitaka jamii kuona umuhimu wa kushiriki zoezi la kujiandikisha kwa wale wenye sifa za kufanya hivyo ili kupata fursa ya kugombea nafasi za Uongozi ngazi ya Mtaa pamoja na kupiga kura.

"Niwaombe sana Wanatunduma, ni muhimu sana, nendeni mkajiandikishe na kujiorodhesha kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura ili muwe sehemu ya uamuzi wa busara ya kuwapata viongozi watakaotuongoza kwa miaka mitano." Amesema Mhe. Chongolo na kuongeza;

"Miaka mitano ni miaka mingi, tusifanye uamuzi kwa kukurupuka, tusifanye uamuzi kwa kushawishiwa vinginevyo, tufanye uamuzi kwa kutambua na kujua tunachokitaka na kuamua ili tukipate kupitia uongozi tutakaouweka kuendelea kutuongoza kwa kipindi cha miaka mitano."

Mhe. Chongolo amesema msingi wa Serikali ya miaka mitano inayokuja, unajengwa kwenye Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, hivyo amewasihi Wananchi wasiache kutumia fursa hiyo vizuri kwa Uandikishaji umeanza tangu tarehe 11 Oktoba 2024 na mwisho ni tarehe 20 Oktoba 2024.

"Sote ni mashahidi wa mambo makubwa ya maendeleo yanayofanywa na Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan, niwaombe twendeni tukashiriki zoezi hili kikamilifu, ili tuwe sehemu ya maamuzi ya busara, tusiache tukaamriwa, tuwe sehemu ya maamuzi." Amesema Mhe Chongolo.

Aidha, Mhe. Chongolo ameitaka jamii kuwa utamaduni wa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili wawe na afya bora na kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo amesema ndiyo yanayoongoza kwa vifo nchini.

Matukio katika Picha:


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa