• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

SERIKALI IMETANGAZA TOZO MPYA MIAMALA YA SIMU NA BENKI

Imewekwa : September 30th, 2022

Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30 imesema mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).

Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha Sh100 hadi Sh2,999 ni Sh10, kuhamisha Sh3,000 hadi Sh3,999 ni Sh14, Sh4,000 hadi 4,999 ni Sh27, kutuma Sh5,000 hadi 6,999  ni Sh54, kutuma Sh7,000 hadi Sh9,999 ni Sh56.

Viwango vingine ni kutuma Sh10,000 hadi 14,999 ni 102, kutuma Sh15,000 hadi 19,999 ni Sh195, kutuma Sh20,000 hadi 29,999 ni Sh306, kutuma Sh30,000 hadi 39,999 ni Sh351, kutuma Sh40,000 hadi 49,999 ni Sh419, kutuma Sh50,000 hadi Sh99,999 ni Sh573, kutuma Sh100,000 hadi 199,999 ni Sh707, kutuma Sh200,000 hadi 299,999 ni Sh821.

Nyingine ni kutuma Sh300,000 hadi 399,999 ni Sh838, kutuma Sh400,000 hadi 499,999 ni Sh982, kutuma Sh500,000 hadi 599,999 ni Sh1,245, kutuma Sh600,000 hadi 699,999 ni Sh1,532.

Nyingine ni kutoka Sh700,000 hadi 799,999 ni Sh1,700, kutuma Sh800,000 hadi 899,999 ni 1,500, kutuma Sh900,000 hadi 1,000,000 ni 1,776, kutuma Sh1,000,001 hadi 3,000,000 ni Sh1,875, kutuma Sh3,000,001 na kuendelea 2,000.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Kifungu cha 46A (2) kimeelezea kanuni za marekebisho ya kanuni za tozo ya miamala ya fedha ya kielektroniki za mwaka 2022 na zimeanza kutumika jana Oktoba mosi.

“Kanuni hizi zitajulikana kama kanuni za Marekebisho ya Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki za Mwaka 2022, na zitasomwa pamoja na Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki, 2022 ambazo hapa zitarejewa kama “Kanuni Kuu”.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kanuni Kuu zinarekebishwa katika kanuni ya 3 kwa kufuta tafsiri ya neno “kuhamisha fedha” na badala yake kuweka “kuhamisha fedha” maana yake ni kuhamisha fedha kielektroniki kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji.

Tafsiri hiyo inaendelea kusema, Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo;

“Akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji huyo huyo na akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo.”

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa