Kila tarehe 14 Juni huwa ni siku ya Kitaifa ya Uchangiaji damu duniani. Kwa mwaka 2022 Tanzania ilichagua maadhimisho haya kitaifa kufanyika mkoani Songwe, Wilaya ya Momba katika Halmashauri ya Mji Tunduma
Maadhimisho haya yenye kauli mbiu isemayo Kuchangia Damu ni kitendo cha Mshikamano, tuungane kuokoa maisha kwa mara ya kwanza yamevunja rekodi baada ya makadirio ya uchangiaji wa damu kuzidi kiwango tarajiwa
Akiongea katika Maadhimisho hayo mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Songwe Mhe. Omary Mgumba, amewapongeza sana wanachi wa mkoa wa Songwe kwa kujitokeza na kuchangia damu kwani tendo hilo ni la kuigwa na nilamfano kwa Watanzania wote.
Pamoja na Maadhimisho hayo yemaambatana na utoaji wa vyeti vya utambuzi na shukrani kwa waliochangia damu mara nyingi ndani ya Tanzania kwani kitendo hicho nichakuokoa maisha ya watanzania wengi wenye uhutaji wa damu
Naye Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Fakii Lulandala aliwashukuru sana wageni wote na Wizara ya Afya kwa kuamua maadhimisho hayo makubwa kufanyika Tunduma kwani kuna Halmashauri nyingi sana lakini wakaamua Wilaya ya Momba
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa