• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

TUNDUMA YASHIKA NAFASI YA SITA YA LISHE KITAIFA 2022/2023

Imewekwa : August 29th, 2023

Na William Maganga - Tunduma


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais -TAMISEMI  imetoa takwimu ya tathimini ya saba ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa mwaka 2022/2023

Tathimini hiyo imetolewa Agosti 29,2023 ambapo Halmashauri ya Mji Tunduma imeshika nafasi ya sita (6) kitaifa kati ya Halmashauri mia moja themanini na nne (184), huku mkoa wa Songwe ukishika nafasi ya saba (7) kati ya mikoa ishirini na sita (26) ya Tanzania bara.

Halmashauri ya Mji Tunduma imepanda kwa kasi katika afua za lishe kitaifa kutoka nafai ya 53 Mwaka 2021/2022 hali kufikia nafasi ya 6 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kuifanya kuwa kinara kwa Mkoa wa Songwe

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma Ndugu Philemon Magesa  amesema Tunduma  imeshika nafasi hiyo kutokana na hatua madhubuti za utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe na kutoa elimu shirikishi kwa jamii juu ya lishe kupitia vikundi vya unasihi wa masuala ya lishe katika mitaa yote sabini na moja (71) ya Halmashauri ya Mji Tunduma. Lengo la elimu hiyo ni kuepusha changamoto za lishe duni kama vile udumavu, uzito pungufu na upungufu wa wekundu wa damu kwa wajawazito pia utapiamlo kwa Watoto.

Aidha Bw. Magesa ametaja mojawapo ya kikundi cha unasihi wa lishe ni  Juhudi-Mpemba kinachotoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora, upimaji wa hali ya lishe kwa Watoto na kuwaunganisha Watoto wenye hali duni ya lishe kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Bw. Magesa ameongeza kuwa  katika Kipindi cha robo ya pili (2) na ya tatu (3) ya  2022/2023 jumla ya watoto 1305 kuanzia miezi 0 – 59  katika kata ya Mpemba walipimwa hali zao za lishe kwa kutumia kipimo cha Mzingo wa Mkono (MUAC TAPE) ambapo Watoto 36 walikuwa na utapiamlo huku mtoto mmoja akiwa na utapiamlo mkali. Kwasasa Watoto hao wameunganishwa katika matibabu na wanaendelea kupata matibabu sitahiki.

Kupitia kauli mbiu ya “Lishe ni msingi wa maendeleo sote tuwajibike”, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma ametoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu kwenye suala la lishe kwani ni wajibu wa jamii nzima, kwani ushiriki wao utapunguza matatizo yatokanayo na lishe kama vile udumavu na utapiamlo kwa Watoto.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa