• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Ufahamu Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Majitaka Tunduma

Imewekwa : December 4th, 2023

Na Benton Nollo, Tunduma TC

Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Majitaka katika Mji wa Tunduma umejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani kupitia mradi wa upatikanaji wa maji na mabadiliko ya Tabianchi kwa gharama ya shilingi milioni 482.2.

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ujerumani zimekuwa na ushirkiano wa muda mrefu kupitia Wizara ya Maji nchini Tanzania na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani, BMZ.

Kupitia ushirikiano huo, Shirika la Misaada la Kijerumani – GIZ linatekeleza miradi ya Upatikanaji wa Maji na Mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya mjini hapa nchini Tanzania. Awamu ya Kwanza ya mradi huo ilianza kutekelezwa mwaka 2019 hadi 2022 na Awamu ya Pili imeanza mwaka 2022 hadi 2025 katika kukabiliana na UVIKO – 19 ambapo Halmashauri ya Mji Tunduma ni sehemu ya Wanufaika wa mradi.

Akizungumza katika mahojiano maalum Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Philemon Magesa amesema lengo la mradi huo ni kuboresha afya na usafi wa mazingira na kutokomeza magonjwa ya mlipuko katika Mji wa Tunduma ambapo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo.

Magesa amesema tangu Halamashauri ya Tunduma ianzishwe Mwezi Julai, 2015 suala la majitaka katika Mji huo limekuwa na changamoto kubwa katika udhibiti wake kwa kuwa majitaka yanazalishwa kwa kiwango kikubwa kutokana na kukua kwa mji na kuondezeka kwa shughuli za kiuchumi.

“Majitaka yanazalishwa kwa kiwango kikubwa kwenye kaya za watu, kwenye maeneo ya kibiashara, na hasa ukizingatia Tunduma ni mji wa kibiashara, kwa hiyo kadiri mji unavyokua ndivyo hivyo hivyo na uzalishaji wa taka zote ngumu na maji zinazalishwa kwa wingi…maeneo ambayo tulikuwa tumechagua kwa ajili ya kuhifadhi majitaka hayakuwa na viwango vyenye ubora unaotakiwa kisayansi…hivi karibuni Serikali imeweza kutupatia mradi wa kudhibiti majitaka uliopo Kata ya Kaloleni ambapo tayari umeshakamilika.” Amesema Magesa.

Magesa amesema Halmashauri ya Mji Tunduma inatarajia mradi huo kuwa chanzo cha mapato kwa kuwa wadau wenye magari ya kunyonya majitaka watakapokuwa wanatoa huduma hiyo kwa Wananchi watalipwa hivyo pindi nao wanapokwenda kumwaga majitaka katika eneo hilo kutakuwa na tozo la kuchangia, hivyo Halmashauri itapata mapato kutoka na magari ya majitaka yatakavyokuwa yanakwenda kumwaga majitaka katika mradi huo.

“Mradi huu kwetu ni chanzo kingine cha mapato, hivyo kwa kuwa hii ni fursa ya kuongeza mapato kupitia mradi huu, sisi kama Halmashauri kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 tumetenga fedha kwa ajili ya kununua gari la majitaka la Halmashauri lenye ujazo wa lita 8,000 ambalo litakuwa kazi yake ni kunyonya majitaka kwenye maeneo ambayo wanahitaji huduma hiyo na kupeleka kwenye mradi huo ambao tayari umeshakamilika na upo tayari kutumika.” Amesema Magesa.    

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tunduma, Fatuma Malende amesema mradi huo umetekelezwa na Mkandarasi Entercecon Limited kwa gharama ya shilingi milioni 482.2 chini ya Mhandisi Mshauri BORDA kwa kushirikiana na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini – RUWASA Mkoa wa Songwe.

Malende amesema mradi huo ulijumuisha shughuli za usawazishaji wa eneo la mradi (land scaping), kujenga miundombinu ya uchakataji wa majitaka, kujenga ofisi na choo, uzio, uwekaji wa mfumo wa umeme na kujenga jengo la kukaushia na kutunzia mbolea pamoja na shamba la migomba ya ndizi.

“Mradi huu umetekelezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ya utekelezaji ilianza mwezi Agosti, 2021 hadi Disemba, 2022 na awamu ya pili ilianza kutekelezwa mwezi Aprili, 2023 hadi Juni, 2023, hivyo mradi huu kwa sasa upo katika kipindi cha matazamio hadi mwezi Januari, 2024.” Amesema Malende.

 Kwa niaba ya Wananchi wa Tunduma, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Ayubu Mlimba ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza mradi huo kwa kuwa una manufaa kwa Wananchi wa Tunduma.

Matukio Katika Picha:

Picha zote juu ni muonekano wa Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Majitaka Tunduma.

Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa