• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Utumishi wa Umma ni Kutumika: DC Mwandobo

Imewekwa : March 5th, 2025

Na Benton Nollo, Tunduma TC

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Elias Mwandobo amesema unapochagua kuwa Mtumishi wa Umma ni wazi kuwa umeapa kuwatumikia Wananchi katika eneo lako ambako Serikali imekuajiri.

Mhe. Mwandobo ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo maalum kwa Watumishi wapya ambao wameajiriwa na Serikali hivi karibuni katika Halmashauri ya Mji Tunduma, ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Halmashauri hiyo tarehe 05 Machi 2025.

"Niwaambie, kufanya kazi serikalini ni heshima kubwa sana, na ukitaka kuona umuhimu wa hilo angalia nchi yetu ina takriban Watanzania zaidi ya milioni 60 kwa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 lakini umeaminiwa wewe, ukaajiriwa...hivyo siyo jambo dogo." Amesema Mhe. Mwandobo na kuongeza;

"Utumishi wa Umma ni mchakato, mpaka nyie mmepatikana ina maana kuna michakato ya kuchujwa mmepitia...msilichukulie jambo hilo kwa wepesi, linauzito wake na ukitambua uzito huo utawajibika ipasavyo katika sehemu yako ya kazi ili kuleta matokeo chanya ambayo ndiyo matarajio ya Mwajiri wetu ambaye ni Serikali."

DC Mwandobo amesema mafunzo yanayotolewa, ni wajibu wa Serikali ambao huutimiza kwa kila anayeingia kuwatumikia Watanzania ili iwe dira katika kutekeleza majukumu husika kwa umma.

Aidha, Mheshimiwa Mwandobo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watumishi hao kuwa, katika utekelezaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali.

"Unapoamua kuja katika utumishi wa umma, tambua kuna Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ambayo ni lazima uifuate...hivyo, hatma ya utumishi bora ipo mikononi mwako...mnafundishwa leo ili msikiuke." Amesema Mhe. Mwandobo.

Halmashauri ya Mji Tunduma kupitia Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasirimali Watu imeendesha mafunzo hayo ya siku moja kwa Watumishi wote wa ajira mpya kupitia Wakufunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa - Hombolo, Dodoma.

Matukio katika Picha:









Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa