• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Wapo Wanaodhani Rais Samia Hapaswi Kupongezwa: DC Kihongosi

Imewekwa : March 30th, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Kenani Kihongosi ameitaka jamii kuona umuhimu wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuwatumikia Watanzania kwa kuleta fedha nyingi za miradi.

Kihongosi ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Momba wakati wa Kongamano la maadhimisho ya miaka mitatu ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambalo limefanyika kwenye Ukumbi wa High Class ya Juu mjini Tunduma tarehe 30 Machi 2024.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali ya Awamu ya Sita inapaswa kupongezwa kwa sababu katika kipindi cha miaka mitatu Wilaya hiyo imepokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu, maji, kilimo na miundombinu mbalimbali.

“Kwa niaba ya Serikali tunamshukuru Rais wetu kwa kutuletea fedha nyingi katika Wilaya yetu ya Momba, lazima tutambue Wilayah ii ina Wilaya 139 na ina Halmashauri 184 lakini Halmashauri hizo zote Serikali imekuwa ikipeleka fedha siyo jambo dogo ni jambo kubwa.” Alisema Kihongosi na kuongeza;

“Wapo baadhi ya watu huwa wanasema kwa nini mnampongeza, wapo wengine huwa wanahisi na kudhani kwamba kiongozi wetu, Rais wetu hapaswi kupongezwa…yeyote ambaye amepewa wito wa kuwatumika Wananchi lazima apongezwe pale anapofanya vizuri…mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.”

Akiwasilisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mwanaisham Nassor alisema Halmashauri ya Mji Tunduma imepokea shilingi bilioni 45.499 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo mapato ya ndani ni shilingi bilioni 17.544 na Serikali Kuu ni shilingi bilioni 2.955.

Nassor alisema kwa upande Elimu Msingi kwa kipindi hicho imepokea shilingi bilioni 7.248 ambazo zimetumika kujenga shule mpya 27, vyumba vipya vya madarasa 200, matundu ya vyoo mapya 373 na kutengeneza madawati mapya 4,863.

Ambapo amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita Halmashauri ya Mji Tunduma ilikuwa na Shule za Msingi 25 wakati kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri hiyo ina shule za msingi 52, vyumba vya madarasa vilikuwa 350 wakati kwa kipindi hicho tayari kuna vyumba vya madarasa 550, walimu waliokuwepo ni 400 wakati mpaka Desemba 2023 kuna walimu 510.

Nassor aliongeza kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani Machi 2021, Halmashauri ya Mji Tunduma ilikuwa na matundu ya vyoo 610 wakati mpaka Machi 2024 Halmashauri ina matundu ya vyoo 983, madawati yalikuwa 4,705 wakati mpaka kipindi hicho kuna madawati 9,568 na kiwango cha ufaulu Darasa la Saba mpaka kufikia asilimia 94.1 mwaka 2023 kutoka asilimia 78 mwaka 2021.

Kwa upande wa Elimu Sekondari kwa kipindi hicho imepokea shilingi bilioni 15.155 ambazo zimetumika kujenga shule mpya za sekondari 5, Shule mpya za Kidato cha Tano na Sita 4, nyumba za Walimu 9 na Mabweni mpya 7.

Nassor alisema mwezi Machi 2021 kulikuwa na Shule za Sekondari za Serikali 11 ambapo mpaka Machi 2024 kuna Shule za Sekondari za Serikali 16 wakati kwa Kidato cha Tano na Sita zimefikia shule 4 kutoka shule 2 mwaka 2021.

Nassor alisema mwaka 2021 hakukuwa na shule za sekondari za bweni lakini mpaka Machi 2024 yamejengwa mabweni ya Wavulana na Wasichana katika Shule ya Sekondari Namole na Dkt. Samia SH. Alisema mwaka 2021 kulikuwa na nyumba za Walimu 11 wakati mpaka kufikia Machi 2024 kuna nyumba za walimu 20, idadi ya Walimu imeongezeka kutoka 238 mwaka 2021 hadi 290 Machi 2024. Alisema mwaka 2021 kulikuwa na wanafunzi 8,888 wakati mpaka Machi 2024 kuna wanafunzi 11,400, huku kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne kimeongezeka na kufikia asilimia 98.4 kutoka asilimia 95.4 mwaka 2021.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Wananchi, ujenzi wa shule mpya na ongezeko la vyumba vya madarasa vimesaidia kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kufuata huduma ya elimu maeneo ya mbali pia imepunguza mlundikano na utoro wa rejareja...ongezeko la Waalimu pamoja na uboreshaji wa miundombinu mingine ya shule imefanya kiwango cha ufaulu kuongezeka.” Alisema Nassor.

Katika Sekta ya Afya, Nassor alisema katika kipindi hicho Halmashauri ilipokea shilingi bilioni 6.125 ambazo zimetumika kujenga Vituo vya vipya 5, Zahanati Mpya 4, Hospitali mpya 1 na upatikanaji wa dawa imeongezeka kwa asilimia 10.

Alisema vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 5 mwaka 2021 hadi vifo 3 mwezi Machi 2024 huku vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 27 mwaka 2021 hadi vifo 26 Machi 2024. Kwa upande wa Zahanati zimeongezeka kutoka zahanati 4 mwaka 2021 hadi zahanati 8 Machi 2024, Vituo vya Afya vimeongezeka kutoka kituo cha afya kimoja mwaka 2021 hadi vituo vya afya 6 Mwezi Machi 2024. Alisema mwaka 2021 hakukuwa na Hospitali ya Serikali lakini hadi kufikia Machi 2024 kuna Hospitali moja ya Mji Tunduma.

Nassor alisema huduma za afya zimesaidia kupunguza vifo visivyo vya lazima kwani kuongezeka kwa miundombinu ya Afya kumepunguza kero ya Wananchi kutembea muda mrefu kutafuta huduma. Aidha, kiwango cha upatikanaji wa dawa kimeongezeka kutoka asilimia 86 na kufikia asilimia 96 hali inayopelekea wagonjwa wengi kuepukana na hali ya kukosa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Sekta ya Kilimo Nassor alisema idadi ya Maafisa ugani kilimo na mifugo walikuwepo 26 mwaka 2021 na hadi Machi 2024 kuna Maafisa ugani kilimo na mifugo 28. Kwa upande wa vitendea kazi mwaka 2021 kulikuwa na pikipiki moja lakini mpaka kufikia Machi 2024 Halmashauri ina pikipiki 32 huku utolewaji wa mbolea ya Ruzuku mwaka 2021 ulikuwa ni kwa baadhi ya wakulima lakini mpaka Machi 2024 Wakulima 11,800 wamepatiwa mbolea ya ruzuku.

Kadhalika, kwa sekta ya viwanda mwaka 2021 kulikuwa na viwanda vidogo vipatavyo 439 ambavyo ni vya kusindika mazao ya mpunga, mahindi, alizeti useremala, kuchomelea na ushonaji lakini mpaka kufikia Machi 2024 Halmashauri ina viwanda vidogo 451 ambapo kuna ongezeko la idadi ya viwanda 102 ambavyo vimezalisha ajira mpya kwa vijana wapatao 306.

Kwa upande wa uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2024 shilingi bilioni 3.8 zilitengwa kwa ajili ya mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya ujasiriamali ya wanawake, vijana na walemavu kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani na marejesho. Nassor alisema kwa kipindi hicho jumla ya shilingi bilioni 2.8 zimekopeshwa kwa vikundi 178 (Wanawake vikundi 75, Vijana vikundi 69 na Walemavu 34).

Amefafanua kuwa mwaka 2021 idadi ya vikundi vya Wanawake,Vijana na wenye ulemavu ilikuwa ya wastani kujitokeza kukopa mikopo ambapo kulikuwa na vikundi 167, kati yake vikundi vya wanawake 99, vikundi vya vijana 54 na Watu Wenye Ulemavu 14 vilijitokeza kuomba mikopo na kufanikiwa kukopeshwa ilhali mpaka kufikia Machi 2024 ongezeko ni kubwa la uundaji wa vikundi kufikia vikundi 336 kati yake vikundi vya wanawake ni 171, vikundi vya vijana ni 120 na Watu Wenye Ulemavu ni 45 hii ni kutona na kuongezeka kwa hamasa juu ya utoaji wa mikopo katika Halmashauri kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Nassor alisema utoaji wa mikopo bila riba umesaidia wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kujiinua kiuchumi, kukuza vipato vyao na imesaidia kutoa ajira kwa vijana ambao hawakuwa na kazi za kufanya mfano utoaji wa pikipiki kwa vijana na vijana wanaojishughulisha na shughuli za kitaalamu hasa upimaji wa ardhi.

Mbali na hayo, Nassor alisema katika kipindi cha Machi 2021 Halmashauri ya Mji haikuwa na Gari la Zomamoto lakini mpaka kufikia Machi 2024 imefanikiwa kununua Gari la Zimamoto jipya aina ya HOWO lenye namba za Usajili SM 15681.

Kabla ya Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Momba mapema asubuhi aliongoza mazoezi (jogging) ya asubuhi ambayo yalianzia Mzunguko wa Mpakani (Border) na kuishia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.

 Aidha, baada ya Kongamano hilo Mkuu huyo wa Wilaya aliandaa futari maalum na kuwafuturisha Waumini wa Dini ya Kiislam ambao wapo katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwenye Ukumbi wa High Class ya Juu mjini Tunduma.

Matukio katika Picha:

(Picha Zote na Benton Nollo)


Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Maonesho ya Fani za Ndani Yafana

    May 26, 2025
  • Mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Songwe Rarindima

    May 26, 2025
  • Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Wawasili Tunduma

    May 26, 2025
  • 'Hii Tunashinda kwa Kishindo'

    May 25, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa