• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
TUNDUMA TOWN COUNCIL
TUNDUMA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mipango
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijijini
      • Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Lishe bora kwa Afya imara
      • Mapambano dhidi ya Malaria
      • Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya
      • Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
    • Huduma ya Elimu
      • Huduma ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Huduma ya Elimu ya Sekondari
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya Kilimo
    • Huduma ya Mifugo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Uchumi, Mipango Takwimu
      • Kamati ya Elimu, Afya na maji
      • Kamati ya Kazi, Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Ethics Committee
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Instagram
    • Facebook
  • Nyaraka
    • Nyaraka
    • Miongozo

Wasimamizi Wasaidizi Ngazi ya Kata, Mtaa, Waandikishaji Wapiga Kura Waapisha, Kupatiwa Mafunzo

Imewekwa : October 2nd, 2024

Na Benton Nollo, TTC

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo amesimamia zoezi la uapishwaji na utoaji wa mafunzo maalum kwa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata (15), Mitaa (71) na Waandikishaji Wapiga Kura takribani 196.

Mafunzo hayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC mjini Tunduma tarehe 02 Oktoba 2024, yakilenga kuwaandaa Wasimamizi hao kusimamia mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Chaurembo amewasisitiza Washiriki hao kuzingatia kiapo chao kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa kwa kuzingatia umuhimu wa ushiriki wa Wananchi katika uchaguzi.

Msimamizi huyo alitoa maelekezo ya kina kuhusu taratibu za uchaguzi, ikiwemo sifa za kugombea, sifa za wapiga kura, na mchakato wa kujiandikisha kupiga kura.

Alibainisha kuwa Wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi, huku wasimamizi wakihakikisha kuwa mchakato mzima unaendeshwa kwa uwazi na haki.

Chaurembo kwa kushirikiana na Waratibu wa Uchaguzi ngazi ya Halmashauri  walieleza na kufafaanua kwa kina Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024, michakato ya kufuatwa na Wasimamizi wa Uchaguzi katika kuhakikisha haki na uwazi vinafikiwa.

Chaurembo ametoa wito kwa Washiriki hao kuhakikisha kuwa kila hatua inazingatia miongozo iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, tarehe 15 Agosti 2024, kama Mwongozo wa uchaguzi wa mwaka huu (2024).

Katika mafunzo hayo, Wasimamizi Wasaidizi walipata fursa ya kula kiapo cha uaminifu, kiapo ambacho kinawataka kuwa waaminifu na waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kusimamia uchaguzi. Kiapo hicho ni sehemu muhimu ya maandalizi ya kuhakikisha kuwa wasimamizi wanafuata sheria na taratibu wakati wote.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi muhimu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024, ambapo Wananchi wa Tunduma na maeneo mengine nchini watapata fursa ya kugombea na kuchagua viongozi watakaowaongoza katika Mitaa yao.

Matukio katika Picha:

Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Momba, Mhe. Timothy Lyon akitoa maelezo kabla ya kuwaapisha Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata (15), Mitaa (71) na Waandikishaji Wapiga Kura takribani 196 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Mji Tunduma, tukio ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 02 Oktoba 2024.

Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata, Mitaa na Waandikishaji Wapiga Kura wakila kiapo cha uaminifu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Momba, Mhe. Timothy Lyon,  kwa ajili ya kushiriki shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Mji Tunduma, tukio ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 02 Oktoba 2024.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo akizungumza wakati wa Semina kwa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata, Mitaa na Waandikishaji Wapiga Kura kwa ajili ya kushiriki shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Mji Tunduma, tukio ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 02 Oktoba 2024.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Tunduma, wakiwasilisha mada mbalimbali kwa nyakati tofauti wakati wa Semina kwa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata, Mitaa na Waandikishaji Wapiga Kura kwa ajili ya kushiriki shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri hiyo, tukio ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 02 Oktoba 2024.

Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata, Mitaa na Waandikishaji Wapiga Kura wakisikiliza kwa makini mafunzo wakati wa semina kwa ajili ya kushiriki shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Mji Tunduma kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Tunduma TC tarehe 02 Oktoba 2024. (Picha zote na Julius Evandino).



Matangazo

  • Tangazo la Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 May 14, 2025
  • Orodha ya Majimbo Mapya na Yaliyobadilishwa Majina May 12, 2025
  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Watahiniwa 694 Kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita 2025 May 03, 2025
  • Taarifa kwa Umma February 27, 2025
  • Onyesha Zote

Habari mpya

  • Mashindano ya UMISSETA Ngazi ya Halmashauri Yaanza Rasmi

    June 02, 2025
  • DAS Nkinda: Ziara ya Viongozi DR Congo Ina Manufaa Tunduma, Taifa

    May 30, 2025
  • Tunduma TC Yang'ara Mpira wa Miguu, Kwaya, Bongo Fleva UMITASHUMTA

    June 28, 2025
  • Dkt. Kasululu Ahitimisha Mashindano ya UMITASHUMTA

    May 28, 2025
  • Onyesha Zote

Maktaba ya video

Ubunifu mkoa wa Songwe
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Songwe Shindani Blogspot
  • Watumishi Portal
  • Tunduma yapata hati Inayoridhisha
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2019
  • Tangazo la kazi sekta ya Afya
  • Sherehe za Muungano
  • Kibali cha Matangazo

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti ya Mkoa wa Songwe
  • OR-TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Msampania, Chapwa - Tunduma

    Sanduku la Posta: P. O. BOX 73

    Simu ya Mezani: +255 25 2957388

    Simu ya Mkononi: +255 756 427 307

    Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa