UTANGULIZI
Shule ya Sekondari Mpemba ilianzishwa mwaka 2006 kwa usajili wa namba S.2303 na ni moja kati ya shule tisa (09) za Serikali katika Halmashauri ya Mji Tunduma. Shule ina jumla ya wanafunzi 707, kati yao wanafunzi 663 ni kidato cha I hadi kidato cha IV ambapo wavulana ni 374 na wasichana ni 289, na kidato cha V ni wasichana 44 pekee. Shule ina jumla ya walimu 33, kati yao wanaume ni 15 na wanawake ni 18.
UTEKELEZAJI WA MRADI
Shule kupitia kamati mbalilmali za ujenzi ziliyoundwa na wananchi kutoka katika kila mtaa ndani ya kata ilianza kutekeleza ujenzi wa mradi huu mwezi Februari mwaka 2018 na mpaka sasa mradi huu umekamilika kwa asilimia miamoja. Miundo mbinu hii ilielekezwa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha Tano ambao kwa Mwaka huu wa masomo waamesharipoti wanafunzi 44 na wanaendelea na masomo yao.Wanafunzi hawa ni wa michepuo ya sanaa yaani HGL na HKL.
UJENZI WA JENGO LA UTAWALA
Jengo hili limekamilika na linatumika. Limetumia jumla ya shilingi 76,247,964. Katika fedha hizi, shilingi 16,247,964 ni fedha kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi 60,000,000 ni fedha toka Serikali Kuu (P4R). Jengo hili lina jumla ya vyumba 09 na vyoo vitano kwa ajili ya walimu.
UJENZI WA MABWENI MAWILI YA WANAFUNZI
Mabweni mawili yamekamilika ambapo kila bweni lilitengewa kiasi cha shilingi 75,000,000. Hivyo mabweni yote mawili yalitengewa shilingi milioni 150,000,000. Mabweni haya yana jumla ya vyumba ishirini kila moja na kila chumba kina uwezo wa kubeba wanafunzi wanne (04) hivyo kila bweni lina uwezo wa kubeba wanafunzi 80.Vilevile mabweni haya yana vyoo vitano na mabafu matano kila moja na sehemu maalumu ya kufulia (laundry).
UJENZI WA BWENI NAMBA 01
Bweni hili limeshakamilika na linatumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano walioripoti mwezi Julai, 2019. Ujenzi wa bweni hili umegharimu shilingi 101,303,000 kati ya fedha hizi, sh 75,000,000 ni fedha toka Serikalini Kuu (P4R) na sh 26,303,000 ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
UJENZI WA BWENI NAMBA 02
Bweni hili limekamilika na limegharimu sh 101,303,000 kati ya fedha hizi, sh 75,000,000 ni kutoka Serikali Kuu (P4R) na sh 26,303,000 ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
UJENZI WA MATUNDU 8 YA VYOO VYA WANAFUNZI
Ujenzi wa matundu ya vyoo umekamilika ambapo matundu 08 ya vyoo badala ya matundu 05 kama mradi ulivyoelekeza yamejengwa, pia chumba kimoja maalumu kwa ajili ya watoto wa kike kimejengwa. Ujenzi huu umegharimu shilingi 7,846,036, kati ya fedha hizi, shilingi 5,500,000 ni fedha kutoka Serikali Kuu (P4R), na shilingi 2,346,036 ni mapato ya ndani ya Halmashauri.
LENGO LA MRADI NA MANUFAA YAKE
Lengo la mradi huu ni kupanua wigo wa utoaji elimu katika jamii ya wananchi wa Tunduma, Mkoa wa Songwe na Tanzania kwa ujumla kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa watoto wa kike wanaofaulu, ili waweze kujiunga na kidato cha Tano (form v) katika Shule za Serikali. Hivyo wanufaika wa mradi huu ni wanajamii wote wa Mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe na Taifa kwa ujumla kwasababu wanafunzi waliojiunga kidato cha tano kwa Mwaka huu wa masomo wametoka maeneo tofauti tofauti ya nchi yetu ya Tanzania.
USHIRIKI WA NGUVU ZA WANANCHI
Mradi huu umefanikiwa kushirikisha nguvu za wananchi wa Kata ya Mpemba katika kazi zifuatazo;
(a)Kuchimba msingi wa majengo yote wakati wa kuanza kwa mradi huu
(b)Kuchimba mashimo yote makubwa na madogo ya vyoo
(c)Kuchota maji ya kujengea kila siku tangu ujenzi ulipoanza hadi ulipokamilika.
Kazi zote hizi zimegharimu kiasi cha sh 10,000,000
MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI
Halmashauri ya Mji wa Tunduma kupitia mapato yake ya ndani, iliwezesha ujenzi huu kukamilika kwa kuongeza kiasi cha shilingi milioni 101,200,000.
HITIMISHO
Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuli kwa kutupatia mradi huu mkubwa sana katika shule ya Sekondari mpemba, Kata ya Mpemba, Vilevile tunaishukuru Halmashauri ya Mji Tunduma kupitia Mkurugenzi wake kwa kutupatia fedha za kukamilisha mradi huu na kwa ushirikiano mkubwa waliotuonyesha tangu mradi ulipoanza hadi ulipokwisha. Mwisho tunawashukuru wananchi wa Kata ya Mpemba kwa ushiriki wao wa hali na mali katika kazi zote walizozifanya. Tunaahidi kufanya vizuri ili kiutangaza shule ya sekondari Mpemba na Halmashauri yetu kwa ujumla.
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa