UTANGULIZI
Halmashauri ya Mji Tunduma Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2018/2019 ilitengewa fedha kwa ajili ya mradi wa Kimkakati yaani Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka mpaka wa Tanzania –Zambia.
HISTORIA YA MRADI
Eneo hili la ujenzi wa Maegesho lina jumla ya ukubwa wa ekari 17 ambazo Halmashuri ilitwaa kutoka kwa wananchi kwa kuwalipa fidia ili kufanikisha Ujenzi wa Mradi huu pamoja na ujenzi wa ofisi nyingine za taasisi.
LENGO LA MRADI
Lengo la Mradi huu ni kuiongezea Halmashauri mapato yake ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka Serikali kuu na hatimaye kujitegemea kabisa katika uendeshaji wake.
GHARAMA ZA MRADI
Halmashauri ya Mji Tunduma ilitengewa fedha jumla ya shilingi 1,630,000,000.00 kutoka serikali kuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania-Zambia kama mradi wa Kimkakati. Pia katika mapato yake ya ndani ilitenga Shilingi 119,000,000 kwa ajili ya kulipa fidia ya kutwaa eneo la kujenga mradi huu kutoka kwa wananchi.
Hadi sasa kiasi cha fedha kilichopokelewa na Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ni shilingi 375,528,516.67 sawa na asilimia 23 ya fedha yote ya mradi, na kuifanya Halmashauri kuingia mkataba na SUMA JKT NYANDA ZA JUU KUSINI wenye thamani ya shilingi 1,628,808,150.45 bila VAT kwa awamu hii ambayo inajumuisha ujenzi wa uzio, jengo la choo, vibanda viwili vya kukusanyia ushuru, ujenzi wa mifereji na sehemu ya kuegesha Magari (Rigid Pavement). Mradi huu awali ulikuwa wa kuegesha magari 45 hadi 75 tu kwa siku lakini baada ya kikao cha wataalam wa Halmashauri (CMT) kukaa tarehe 30/04/2019 kiliamua ufanyiwe mapitio mkataba kwa lengo la kuongeza ukubwa wa eneo ili liweze kuegesha magari mengi zaidi. Baada ya kikao hicho Timu ya wataalam ilifanya kazi ya mapitio (Re-Design) na kuongeza eneo la kuegesha magari kuanzia magari 105 kwa siku.
Mradi mzima wa kujenga Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania-Zambia mpaka utapokamilika tunatarajia utagharimu zaidi ya shilingi bilioni nane (Tshs.8bil) ambao utajumuisha eneo la Maegesho (pavement) la kuegesha Magari zaidi ya 300, Mgahawa wa chakula (Reustaurant), Vyoo vya kulipia (Ablution blocks), uzio wa tofari (Fence), Nyumba za kupumzika madereva na Makondakta (Rest house).
Hata hivyo tayari ujenzi umeshaanza kutekelezwa na jumla ya shilingi 375,528,516.67 zimeshatumika kumlipa mkandarasi malipo ya awali (advance payment) na hati ya kwanza ya malipo (1st Cert).Aidha kiasi cha Shilingi 99,000,000.00 kutoka mapato ya ndani kimeshalipwa kwa wananchi kama fidia ya kutwaa eneo la ujenzi huu na kiasi kilichobakia cha Shilingi 20,000,000.00 kitalipwa robo hii ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/2020.
Aidha mkataba huu ulisainiwa tarehe 22/01/2019 na ulikuwa wa siku 180 hivyo ulitarajiwa kukamilka 22/07/2019. Baada ya hapo Mkandarasi akaomba ongezeko la muda wa siku 91 lakini kulingana na sababu alizotoa zikapelekea kupatiwa siku 45 tu na hivyo kutakiwa kukabidhi mradi ifikapo tarehe 6/09/2019.
MANUFAA YA MRADI
Manufaa ya mradi huu wa Ujenzi wa Maegesho ya Magari Makubwa yanayovuka Mpaka wa Tanzania–Zambia (Truck’s Parking) ukikamilika tunatarajia utaiongezea Halmashauri mapato kwa kiasi cha Shilingi za kitanzania 191,625,000.00 kwa mwaka kwa magari 105. Na mradi mzima utakapokamilika kwa hatua zote tunatarajia utaiongezea Halmashauri Mapato kwa kiasi cha fedha za kitanzania shilingi 547,500,000.00 kwa mwaka kwa magari 232 na kuongeza ajira kwa vijana hususani katika sekta ya Usafi na Mazingira.
KAZI ZILIZOFANYIKA
Katika utekelezaji wa mradi huu kwa awamu hii kazi ambazo zimeshatekelezwa mpaka sasa ambazo ni sawa na asilimia hamsini na tano (55%) ni pamoja na:-
HITIMISHO
Msampania, Chapwa - Tunduma
Sanduku la Posta: P. O. BOX 73
Simu ya Mezani: +255 25 2957388
Simu ya Mkononi: +255 752 807 767
Barua Pepe: td@tundumatc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya mji Tunduma. Haki zote zimehifadhiwa